Pata taarifa kuu

Biden amtaka Netanyahu kutumia 'mpango' wa "kuhakikisha usalama" wa raia Rafah

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumapili amemtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutofanya operesheni ya kijeshi huko Rafah, katika Ukanda wa Gaza, "bila mpango unaoaminika na unaowezekana" wa kulinda raia, Ikulu ya White House imesema.

Wapalestina hawa wakiomboleza vifo vya ndugu na marafiki zao waliouawa katika mashambulizi ya Israel, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 10, 2024.
Wapalestina hawa wakiomboleza vifo vya ndugu na marafiki zao waliouawa katika mashambulizi ya Israel, huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 10, 2024. © Ibraheem Abu Mustafa / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Katika simu, rais wa Marekani "amethibitisha maoni yake kwamba operesheni ya kijeshi katika Rafah haipaswi kufanyika bila mpango wa kuaminika na kufikiwa ili kuhakikisha usalama (...) wa zaidi ya watu milioni moja wanaokimbilia huko," serikali ya Marekani imesema katika taarifa.

UNRWA inasema usafirishaji wa misaada umezuiwa katika bandari ya Israel

Shirika kuu la Umoja wa Mataifa linalotoa msaada kwa Wapalestina huko Gaza (UNRWA) linakabiliwa na vikwazo vinavyoongezeka vya utawala kutoka Israel. Shehena ya chakula cha mwezi mmoja imekwama bandarini, mkuu wa shirika hilo Philippe Lazzarin amesema.

Kutokana na hali hiyo, shehena kutoka Uturuki, yenye makontena 1,049 ya vifaa vikiwemo unga, mbaazi, sukari, mafuta ya kupikia, ya kutosha kukidhi mahitaji ya watu milioni 1.1 kwa mwezi mmoja, ilizuiwa bandarini, alitangaza Philippe Lazzarini siku ya Ijuma. Aliongeza kuwa UNRWA iliifahamisha Uturuki kuhusu kizuizi hiki. Mamlaka ya Uturuki haikutoa maoni yoyote mara moja.

Msemaji wa wizara ya fedha amesema suala hilo liko mikononi mwa mshauri wa sheria wa serikali, lakini hakutoa maoni zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.