Pata taarifa kuu

Shinikizo la kimataifa laongezeka kuhusu makubaliano kati ya Israel na Hamas

Shinikizo la kimataifa limeongezeka siku ya Jumanne kwa makubaliano ya usitishaji vita kati ya Israel na Hamas ikiwa ni pamoja na kuachiliwa upya kwa mateka, licha ya vitisho vya mashambulizi dhidi ya Rafah, kimbilio la mwisho la Wapalestina zaidi ya milioni moja katika Ukanda wa Gaza.

Mwanamke akipita mbele ya picha za mateka zilizobandikwa ukutani huko Tel Aviv mnamo Februari 12, 2024.
Mwanamke akipita mbele ya picha za mateka zilizobandikwa ukutani huko Tel Aviv mnamo Februari 12, 2024. AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu

■ Rais wa Marekani Joe Biden amemsihi Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu "kuhakikisha usalama" wa wakazi wa Palestina huku mataifa kadhaa yakionya kuhusu "janga la kibinadamu" katika tukio la shambulio dhidi ya jiji hilo lenye wakazi wengi.

■ Joe Biden alitangaza kwamba makubaliano ya kuwaachilia mateka wanaoshikiliwa huko Gaza, yakiambatana na kusitishwa kwa "angalau wiki sita" katika uhasama kati ya Israel na Hamas, yamekuwa yanajadiliwa kwa sasa.

■ Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema aliamuru jeshi kuandaa mpango wa kuwahamisha raia kutoka Rafah, ambapo anapanga kuanzisha "operesheni kubwa" na kushinda vita vya mwisho vya Hamas.

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya Hamas, iliyotolewa leo Jumanne, Februari 13, watu 28,473 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, 2023. Wizara hiyo imeripoti jumla ya vifo 133 katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Wahanga wengi ni wanawake, vijana na watoto. Pia Watu 68,146 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita hivyo, wizara ya Afya ya Palestina imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.