Pata taarifa kuu

Wanajeshi watatu wa Marekani wauawa Jordan, Joe Biden aishushia lawama Iran

Rais wa Marekani Joe Biden anaripoti katika taarifa yake kwamba wanajeshi watatu wa Marekani walipoteza maisha katika kambi ya kijeshi huko Jordan: “Jana usiku, wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa, na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya vikosi vyetu vilivyoko Jordan kaskazini mashariki mwa Jordan. "

Rais wa Marekani Joe Biden, katika misa katika Kanisa la St. John-Baptista huko Columbia, Souht Carolina, Jumapili hii, Januari 28, 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden, katika misa katika Kanisa la St. John-Baptista huko Columbia, Souht Carolina, Jumapili hii, Januari 28, 2024. AFP - KENT NISHIMURA
Matangazo ya kibiashara

 

Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Marekani kuuawa katika eneo la Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza.Rais Joe Biden ametishia kulipiza kisasi dhidi ya wahusika wa shambulio hili la ndege zisizo na rubani. Marekani "itaendeleza ahadi yake ya kupambana na ugaidi." Na msiwe na shaka: tutawawajibisha wale wanaohusika wakati na jinsi tutakavyochagua. "

"Wakati bado tunakusanya shahidi kuhusu shambulio hili, tunajua kwamba lilifanywa na makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali wanaoungwa mkono na Iran yanaoendesha harakazi zao nchini Syria na Iraq. Jill na mimi tunaungana na familia na marafiki wa waliofariki - na Wamarekani kote nchini - katika kuomboleza vifo vya wapiganaji hawa katika shambulio hili la baya na la kijinga na lisilo la haki kabisa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.