Pata taarifa kuu

Netanyahu apinga 'uhuru wa Palestina' Gaza yaendelea kukumbwa na mapigano makali

Wakati Israel inaelekeza shughuli zake kusini mwa Ukanda wa Gaza, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu Jumamosi, Januari 20, alikataa pendekezo la Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu suluhisho la mataifa mawili katikati mwa mzozo unaoendelea katika ya Israel na Palestina. Siku ya Jumamosi jioni, kambi ya muungano wa kimataifa dhidi ya Daesh ililengwa magharibi mwa Iraq.

Moshi unapanda juu ya Khan Younes, ambako mapigano yanapamba moto, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumapili hii, Januari 21, 2024.
Moshi unapanda juu ya Khan Younes, ambako mapigano yanapamba moto, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumapili hii, Januari 21, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Israel inaendelea na mashambulizi makali kusini mwa Ukanda wa Gaza. Israeli pia inaendelea kufanya operesheni katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

■ Baada ya mazungumzo ya simu kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Joe Biden, Netanyahu alithibitisha tena siku ya Jumamosi upinzani wake kwa "uhuru wa Palestina" huko Gaza. Netanyahu alimwambia mshirika wake Marekani kwamba hakubaliani na pendekezo lake.

■ Shambulio la Israel huko Damascus, mji mkuu wa Syria, liliua watu kumi siku ya Jumamosi, wakiwemo wanajeshi watano wa kikosi ch walinzi wa Mapinduzi na hasa mkuu wa idara ya uasusi la Iran nchini Syria na naibu wake. Wanamgambo wa Iraq kisha walirusha makombora katika kambi ya Marekani nchini Iraq.

■ Wakati Umoja wa Ulaya ukitoa ishara zinazokinzana kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, kwa kuiwekea vikwazo Hamas pia kwa kuanzisha shutuma dhidi ya Israel, mkutano utafanyika Jumatatu mjini Brussels na mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya na wenzao sita katika eneo hilo.

■ Kulingana na ripoti iliyotangazwa Jumapili hii, Januari 21 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 25,105 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Zaidi ya watu 62,681 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.