Pata taarifa kuu

Israel yazidisha mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi

Israel inaendelea na kuzidisha mashambulizi yake huko Khan Younes Januari 18, mji mkuu kusini mwa Ukanda wa Gaza. Jeshi pia linaendelea na mashambulizi yake katika Ukingo wa Magharibi.

Katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Rafah, Januari 18, 2024.
Katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Rafah, Januari 18, 2024. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA
Matangazo ya kibiashara

 

Israel inashutumiwa kwa kulenga kundi la raia wa Palestina wasio na uhusiano na makundi yenye silaha na ambao hawakuwa tishio kwa vikosi vya Israel, kwa mujibu wa mashahidi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Wanaume saba - wanne kati yao ndugu - waliuawa katika shambulio la anga la Israeli mapema Januari 7, walipokuwa wameketi karibu na barabara ya kijiji cha al-Shuhada, kilomita 10 kutoka mji wa Jenin.

Wakati huo huo jeshi la Marekani limewalenga Wahouthi katika eneo lao nchini Yemen kwa mara ya nne katika muda wa chini ya wiki moja.

Watu wawili wameuawa katika shambulio la bomu karibu na Khan Younes

Shambulio la bomu lililofanywa na Israel limeua Wapalestina wawili na kuwajeruhi wengine katika eneo la Abasan, mashariki mwa Khan Yunis, wanahabari wa Al Jazeera wameripoti. Shambulio hilo linakuja siku moja baada ya wapiganaji wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel kushiriki katika mapigano yao makali zaidi huko Khan Yunis kwa miezi kadhaa, kulingana na waangalizi wa vita, na baada ya mashambulizi makali ya Israel kuharibu nyumba na miundombinu zaidi katika eneo hilo.

Mapigano mapya kwenye mpaka wa Israel na Lebanon

Jeshi la Wanahewa la Israel limetangaza kwamba limeshambulia miundombinu ya kundi la kigaidi la Hezbollah katika eneo la al-Adaisa kusini mwa Lebanon, na pia katika kijiji cha Kila na maeneo ya Marj Ayoun. Hapo awali, roketi mbili zilirushwa kutoka Lebanon kuelekea kijiji cha Arab al-Aramsha nchini Israel, na kuanguka katika maeneo ya wazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.