Pata taarifa kuu

Israel: 'Awamu kubwa' ya mapigano kusini mwa Gaza 'itakwisha hivi karibuni'

Awamu kali ya mapigano "inakaribia kutamatika" kaskazini mwa Gaza, Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant amesema. Kwa upande wa kusini, “hii itaisha hivi karibuni,” amehakikisha.

Moshi unapanda juu ya majengo katika Ukanda wa Gaza wakati jua likitua, Jumatatu, Januari 15, 2024.
Moshi unapanda juu ya majengo katika Ukanda wa Gaza wakati jua likitua, Jumatatu, Januari 15, 2024. REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

■ Awamu kali ya mapigano "inakaribia kufikia mwisho" kaskazini mwa Gaza, amesema Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant, akiongeza kuwa kusini, "itakwisha hivi karibuni".

■ Video mpya ya Hamas inatangaza vifo vya mateka wawili wa Israeli. Tawi la kijeshi la Hamas linadai kuwa "waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Wazayuni huko Gaza."

■ Mwanamke mmoja aliuawa na takriban wengine 17 kujeruhiwa katika shambulio la gari huko Ra'anana, katikati mwa Israeli siku ya Jumatatu. Washukiwa wawili wa Kipalestina wanazuiliwa.

■ Kulingana na ripoti iliyotangazwa siku ya Jumatatu, Januari 15 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 24,100 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 60,000 walijeruhiwa. Zaidi ya watoto 10,000 - au 1% ya jumla ya watoto katika Ukanda wa Gaza - wameuawa, kulingana na ripoti mpya kutoka shirika llisilo la kiserikali la Save The Children.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.