Pata taarifa kuu

Gaza: Umoja wa Mataifa washutumu siku 100 za 'vita vya uharibifu'

Katika mkesha wa siku mia moja za mzozo mbaya katika Ukanda wa Gaza, Umoja wa Mataifa umeshutumu "doa juu ya ubinadamu wetu wa pamoja" huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihakikisha kwamba "hakuna mtu" atakayeizuia Israel katika vita vyake vya kuliangamiza kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina. 

Wapalestina wanaomboleza ndugu zao waliouawa katika shambulio la anga huko Rafah, Jumamosi Januari 13, 2024.
Wapalestina wanaomboleza ndugu zao waliouawa katika shambulio la anga huko Rafah, Jumamosi Januari 13, 2024. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

"Imepita siku mia moja tangu vita hivyo vya uharibifu vilipoanza, kuua na kuwafukuza watu huko Gaza, kufuatia mashambulizi ya kutisha ya Hamas na makundi mengine dhidi ya raia wa Israeli. Imekuwa siku mia moja ya shida na huzuni kwa mateka na familia zao,” amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, Philippe Lazzarini, kutoka Palestina.

Huko Tel Aviv, Benjamin Netanyahu amesisitiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari: "Hakuna mtu atakayetuzuia, wala Hague, wala Mhimili wa Uovu, wala mtu mwingine yeyote", hasa akizungumzia ombi la Afrika Kusini mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikiishutumu Israel kwa kitendo cha mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Na kwa mkuu wa majeshi ya Israel kuhakikisha wakati huo huo kwamba nchi yake inaendesha vita vya "haki" ili kutetea "haki yake ya kuishi kwa usalama".

Siku ya Jumamosi, jeshi la Israel limetekeleza tena mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza, ambapo makumi ya watu wameuawa, kulingana na Hamas.

Tangu Ijumaa, mzozo huo umeenea hadi Yemen, na hujuma za Marekani na Uingereza dhidi ya waasi wa Houthi ambao wanashambulia usafiri wa baharini katika Bahari Nyekundu kwa "mshikamano" na Gaza. Mashambulizi mapya yameripotiwa katika bandari wa Hodeida magharibi mwa Yemen siku ya Jumamosi, kulingana na vyanzo vya usalama vya ndani.

Mashambulizi ya Israel kusini mwa Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na makumi ya wengine kujeruhiwa, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Hamas, kundi ambalo limekuwa likidhibiti eneo dogo la Palestina lililozingirwa tangu mwaka 2007 lenye msongamano mkubwa wa watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.