Pata taarifa kuu

Vita vya Hamas na Israel: mzozo unaweza kudumu 'miezi mingi', IDF yasema

Licha ya wasiwasi mkubwa wa kibinadamu, jeshi la Israel limeongeza mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza siku ya Jumatano kama sehemu ya operesheni yake dhidi ya Hamas , huku likibaini kwamba operesheni hiyo inaweza kudumu kwa "miezi mingi zaidi". 

Kifaru cha jeshi la Israel kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza, kusini mwa Israel, huku jeshi likiripoti mapigano makali na Hamas, Oktoba 31, 2023.
Kifaru cha jeshi la Israel kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza, kusini mwa Israel, huku jeshi likiripoti mapigano makali na Hamas, Oktoba 31, 2023. © JACK GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ishara mpya ya kuongezeka kwa mzozo wa kikanda, Marekani imenasa ndege zisizo na rubani katika Bahari Nyekundu na makombora yaliyorushwa na waasi wa Yemen wa Houthi ambao wanatishia maslahi ya Israeli katika "kuunga mkono" Gaza.

Katika eneo hili la Palestina, vikosi vya Israeli "vinapigana huko Khan Younes" (kusini) na "kuendeleza" operesheni zao katika kambi katikati, msemaji wa jeshi Daniel Hagari alisema siku ya Jumanne jioni. Jeshi lilitoa agizo la kuondoka kwa wakaazi wa kambi ya al-Bureij (katikati) na viunga vyake. Baadhi walikuwa tayari wamekimbilia Rafah, ambako waliwasili na mizigo yao ikiwa imerundikwa juu ya magari yao, kulingana na shirika la habari la AFP.

Zaidi ya watu 240 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, wizara ya afya ya Hamas ilisema siku ya Jumanne. Miili ya Wapalestina ilisafirishwa kwa lori hadi kwenye kaburi la pamoja huko Rafah ambako walizikwa, kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. “Tulipokea kontena lililokuwa na idadi kubwa ya wahanga. Baadhi walikuwa miili kamili, wakati kwa wengine baadhi ya viungo vya binadamu,” alilaumu Marwan al-Hams, mkuu wa kamati ya dharura ya afya katika mji wa Rafah. Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena amesema "ana wasiwasi mkubwa juu ya kuendelea kwa mashambulizi ya Israel katikati mwa Gaza" na kutoa wito wa "kutofautisha" kati ya raia na wapiganaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.