Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa wamteua waziri wa Uholanzi kuratibu shughuli za kibinadamu huko Gaza

Umoja wa Mataifa umetangaza siku ya Jumanne, Desemba 26, 2023, uteuzi wa waziri anayemaliza muda wake wa Uholanzi, Sigrid Kaag, katika wadhifa wa mratibu wa mwitikio wa mahitaji ya kibinadamu na ujenzi mpya huko Gaza, kufuatia azimio la Baraza la Usalama kuhusu msaada katika eneo la Palestina linaloshambuliwa kwa mabomu na kuzingirwa na Israeli.

Sigrid Kaag, waziri wa fedha na naibu waziri mkuu katika serikali inayoondoka ya Mark Rutte
Sigrid Kaag, waziri wa fedha na naibu waziri mkuu katika serikali inayoondoka ya Mark Rutte AFP - ERIC PIERMONT
Matangazo ya kibiashara

Sigrid Kaag "atawezesha, kuratibu, kufuatilia na kuthibitisha usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kwenda Gaza" na pia atakuwa na kazi ya "kuanzisha utaratibu wa Umoja wa Mataifa ili kuharakisha usafirishaji wa misaada ya kibinadamu kwenda Gaza kupitia mataifa ambayo sio pande zinazohusika," amesema. msemaji wa Katibu Mkuu Antonio Guterres katika taarifa.

Anatarajiwa kuchukua madaraka Januari 8, ameongeza.

Sigrid Kaag, waziri wa fedha na naibu waziri mkuu katika serikali inayoondoka ya Mark Rutte, ameteuliwa chini ya azimio la Baraza la Usalama lililopitishwa siku ya Ijumaa, ambalo linataka kuwasilishwa kwa misaada "mikubwa" ya kibinadamu huko Gaza, lakini sio kusitishwa kwa mapigano, ambayo Marekani, mfuasi mkuu wa Israel, haitaki.

Vita hivyo vimewalazimu watu milioni 1.9 kukimbia makazi yao katika Ukanda wa Gaza, au 85% ya watu wote kulingana na Umoja wa Mataifa. Njaa inatishia katika eneo hilo na hospitali nyingi hazina huduma.

Misaada ya kimataifa inawasili kwa kiasi kidogo huko Gaza, chini ya mzingiro wa Israeli tangu Oktoba 9 baada ya zaidi ya miaka 16 ya vikwazo vya Israeli.

Takriban miezi mitatu baada ya kuanza kwa vita hivi, vilivyochochewa na shambulio la umwagaji damu lililozinduliwa Oktoba 7 na Hamas nchini Israel, mapigano ya ardhini kati ya wanajeshi wa Israel na wapiganaji wa Palestina, pamoja na mashambulizi mabaya ya anga ya Israel, hayaonyeshi dalili ya kuisha.

Israel iliapa kuiangamiza Hamas baada ya shambulio hili lililotekelezwa na makomandoo waliojipenyeza kutoka Gaza, ambalo lilisababisha vifo vya takriban watu 1,140, ​​wengi wao wakiwa raia, kulingana na takwimu rasmi za hivi punde za Israeli. Takriban watu 250 wametekwa nyara, kulingana na Israel, kati yao 129 wamesalia kizuizini huko Gaza.

Katika operesheni za kulipiza kisasi za kijeshi za Israel huko Gaza, watu 20,915 wameuawa, wengi wao wakiwa wanawake, vijana na watoto, pamoja na 54,918 kujeruhiwa, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.