Pata taarifa kuu

Gaza yakabiliwa na mashambulizi kabla ya kura mpya ya Umoja wa Mataifa ya kusitisha mapigano

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia Jumatatu hii, Desemba 18 kuamua juu ya nakala mpya inayotaka "kusitishwa kwa haraka na kudumu kwa mapigano" huko Gaza, wakati ambapo Washington inaonesha dalili za kukosa subira kwa mshirika wake, Israel.

Timu za matabibu zikikagua uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israeli kwenye wodi ya wajawazito ya Hospitali ya Nasser huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumapili, Desemba 17, 2023.
Timu za matabibu zikikagua uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israeli kwenye wodi ya wajawazito ya Hospitali ya Nasser huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Jumapili, Desemba 17, 2023. © Mohammed Dahman / AP
Matangazo ya kibiashara

Siku kumi baada ya kura ya turufu ya Marekani, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaamua leo Jumatatu juu ya nakala mpya inayotaka "kusitishwa kwa haraka na kudumu kwa mapigano" huko Gaza, wakati ambapo Washington inaonesha dalili za kutokuwa na subira na mshirika wake wa Israel.

Rasimu mpya ya nakala iliyotayarishwa na Falme za Kiarabu, ambayo shirika la habari la AFP iliweza kuona, "inataka kusitishwa kwa haraka na kwa kudumu kwa mapigano ili kuruhusu ufikiaji usiozuiliwa wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza." Hasa, inazitaka pande zinazohusika katika mzozo huo kuwezesha kuingia na kusambaza misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, "kwa nchi kavu, baharini na angani". Rasimu hiyo pia inathibitisha kuunga mkono suluhisho la serikali mbili na "inasisitiza umuhimu wa kuunganisha Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi chini ya mwavuli wa Mamlaka ya Palestina."

Tarehe 9 Desemba, licha ya shinikizo kubwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Marekani ilizuia katika Baraza hilo kupitishwa kwa azimio la kutaka "kusitishwa mara moja kwa mapigano " katika Ukanda wa Gaza. Wiki iliyopita, Baraza Kuu lilipitisha azimio hilihili kwa kura 153, nchi 10 zilipinga na 23 zilijizuia, kati ya nchi 193 wanachama wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa uungwaji mkono huu mkubwa, nchi za Kiarabu zilitangaza jaribio jipya la Baraza la Usalama, matokeo yake bado hayajulikani.

Taarifa kuhusu hali ya Gaza katika ramani

Katika ramani zinazotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Vita, kituo cha utafiti cha Marekani, kinaonyesha kwamba jeshi la Israel linaendelea na operesheni zake kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, karibu na kambi ya Jabaliya na huko Shujaiya. Jana, Jumapili Desemba 17, vikosi vya Israeli pia viligundua "handaki kubwa zaidi" ambalo Hamas imechimba. Taasisi hiyo pia inaeleza kuwa jeshi la Israel lilisonga mbele katikati ya mji wa Bani Suheila, mashariki mwa Khan Younes.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.