Pata taarifa kuu

Marekani yazuia azimio la usitishwaji mapigano la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Marekani imetumia kura yake ya turufu kuzuia azimio la usitishwaji wa mapigano huko Gaza lililopendekezwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Naibu Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Robert A. Wood akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Gaza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Desemba 8, 2023.
Naibu Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Robert A. Wood akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Gaza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Desemba 8, 2023. AFP - YUKI IWAMURA
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana siku ya Ijumaa ili kujadili azimio la usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas. Katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres ametumia Kifungu cha 99 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo lililotayarishwa na Falme za Kiarabu na kuungwa mkono na takriban nchi 100, limepata kura 13 za 'Ndio', kura moja 'Hapana' ya (Marekani), na moja ya Uingereza, ambayo imejizuia kutoa msimamo wake.

Wakati jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza hasa katika miji ya Jabalia na Khan Younis, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeakutana Ijumaa baada ya Katibu Mkuu Antonio Guterres kutumia Kifungu cha 99 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambacho kwa miongo kadhaa hakijatumiwa. Kifungu hicho kinamruhusu katibu mkuu kuwasilisha kwa baraza la Usalama suala lolote ambalo kwa mtazamo wake linaweza kutishia amani na usalama kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.