Pata taarifa kuu

Gaza : Washington inaamini makubaliano yataafikiwa kuhusu kuachiwa huru kwa mateka

Nairobi – Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema anaamini kuna makubaliano yatafikiwa hivi karibuni kuhusu kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza, wakati huu Israel ikizidisha mashambulio dhidi ya kundi hilo.

Kundi la Hamas linawashikiliwa mateka watu 240 iliyowachukua baada ya shambuluio lake la October 7
Kundi la Hamas linawashikiliwa mateka watu 240 iliyowachukua baada ya shambuluio lake la October 7 AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Hamas linawashikiliwa mateka watu 240 iliyowachukua baada ya shambuluio lake la October 7, ambapo waisrael 1200 waliuawa.

Wanajeshi wa Israeli wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika Ukanda wa Gaza tangu wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio dhidi ya ardhi yake
Wanajeshi wa Israeli wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika Ukanda wa Gaza tangu wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio dhidi ya ardhi yake AFP - SAID KHATIB

Msemaji wa baraza la usalama wa taifa, John Kirby, akizungumza na wanahabari hapo jana, amesema bado wanafanyia kazi makubaliano haya, ingawa kuna matumaini makubwa.

‘‘Suala la mateka bado tunalifanyia kazi saa baada ya saa, sina taarifa zaidi kuhusu makubaliano ya kuachiwa kwa matekea lakini tunaamini tunakaribiana kuafikiana makubaliano.’’ alisema John Kirby.

00:39

Msemaji wa baraza la usalama wa taifa la Marekani, John Kirby

Tangu wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio dhidi ya Israeli, mamlaka katika ukanda wa Gaza inasema karibia raia elfu 13 wa Palestina wameuawa katika mashambulio ya Israel wakiwemo watoto zaidi ya elfu tano.

Jarida la Washington Post Jumamosi iliyopita liliripoti kuwa Israel, Marekani na Hamas zilikubaliana kuhusu suala la ubadilishanaji wa mateka wanaozuiliwa na Hamas, wakati mashambulio yakisitishwa kwa kipindi cha siku tano.

Israel imeapa kuwaliza wapiganaji wa Hamas
Israel imeapa kuwaliza wapiganaji wa Hamas © IDF

Wito umekuwa ukitolewa wa kusitishwa mapigano yanayoendelea, China wiki hii ikisema kuwa iko tayari kusaidia katika urejeshaji wa amani katika eneo la Mashariki ya kati.

Wakati wa kikao na waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Beijing Wang Yi, wajumbe kutoka nchi za Kiarabu wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea.  

 

  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.