Pata taarifa kuu

UNRWA: 'Asilimia 40 ya watu sasa wanatishiwa na njaa' Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limepaza sauti kusaidia raia wa katika Ukanda wa Gaza wanaotishiwa na na njaa.

Picha hii iliyopigwa na ndege isiyo na rubani inaonyesha maelfu ya mahema yanayotumiwa na watu waliokimbia makazi yao huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Ijumaa, Desemba 29, 2023.
Picha hii iliyopigwa na ndege isiyo na rubani inaonyesha maelfu ya mahema yanayotumiwa na watu waliokimbia makazi yao huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Ijumaa, Desemba 29, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

"Kila siku ni mapambano ya kuishi, kutafuta chakula na maji. Tunahitaji vifaa vya mara kwa mara na upatikanaji salama na endelevu wa msaada wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza,” linaelezea Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Watatu wafariki katika mashambulizi karibu na Aleppo, Syria, kulingana na OSDH

Shirika lisilo la kiserikali la Syrian Observatory for Human Rights (OSDH) linaripoti kwamba mmashambulizi yaliyotokea karibu na Aleppo, nchini Syria, yaliua watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa. "Makombora ya Israeli" yalilenga "ghala na vituo vya makundi yanayounga mkono Iran" katika eneo karibu na uwanja wa ndege wa mji wa kaskazini mwa Syria. Chanzo cha kijeshi kilichotajwa na sirika la habari la serikali ya Syria, la SANA, kinathibitisha kwamba karibu 5:20 jioni. saa za huko, "adui Israeli amefanya shambulio la anga (...) kulenga baadhi ya maeneo kusini mwa mji wa Aleppo" . Lakini kwa upande wake, linaripoti tu "uharibifu wa nyenzo".

Shambulio linalowezekana kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi karibu na Aleppo, Syria

Israel ilishambulia uwanja wa ndege wa kijeshi wa al-Nairab karibu na mji wa kaskazini mwa Syria wa Aleppo, kwa mujibu wa tovuti yenye uhusiano na upinzani wa Syria na kuripotiwa na kituo cha habari cha Al Jazeera, ambacho kinaongeza kuwa kwa mujibu wa shirika la habari la Lebanon al-Mayadeen, lililo karibu na Hezbollah , mashambulizi manne ya anga yalitekelezwa katika kitongoji cha kusini mashariki mwa Aleppo.

Jeshi la Israeli latoa majina ya wanajeshi wake wawili waliofariki huko Gaza

Wa kwanza alikuwa Constantine Sushko, 30, kutoka Tel Aviv. Aliuawa Jumamosi hii katikati mwa Gaza, kwa mujibu wa jeshi la Israel lililonukuliwa na Gazeti la Haaretz. Kuhusu Harel Ittah, 22, kutoka Netanya, alikufa kutokana na majeraha yake huko Gaza wiki iliyopita, kulingana na chanzo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.