Pata taarifa kuu

Ndege zisizo na rubani zadunguliwa nchini Iran: Tehran na Israel zasalia kimya

Iran imewasha mfumo wake ulinzi wa anga katika majimbo kadhaa mapema Ijumaa Aprili 19 baada ya ripoti za milipuko kadhaa katikati mwa nchi. Maafisa wakuu wa Marekani wameripoti shambulizi la Israel kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel wikendi iliyopita.

Picha iliyopigwa na televisheni ya taifa ya Iran, Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), inaonyesha kile televisheni hiyo inaonyesha kama taswira ya moja kwa moja ya jiji la Isfahan, mapema leo 19 Aprili 2024.
Picha iliyopigwa na televisheni ya taifa ya Iran, Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), inaonyesha kile televisheni hiyo inaonyesha kama taswira ya moja kwa moja ya jiji la Isfahan, mapema leo 19 Aprili 2024. © AFP / HO / IRIB
Matangazo ya kibiashara

Tunachojua:

Tehran iliripoti milipuko mitatu iliyotokea alfajiri siku ya Ijumaa karibu na kambi ya kijeshi katika mkoa wa Isfahan, katikati mwa nchi. Iran mara moja ilianzisha ulinzi wake wa anga katika majimbo kadhaa. Ndege zisizo na rubani zimedunguliwa lakini hakujawa na shambulio la kombora "hadi sasa," mamlaka ya Iran imesema.

Mitambo ya nyuklia iliyo katika eneo la Isfahan ni "salama kabisa", shirika la habari la Tasnim limesema.

Hakuna maoni kutoka kwa jeshi la Israel "kwa sasa" lakini taifa la Kiyahudi lilikuwa limeonya kwamba litalipiza kisasi baada ya Iran kurusha mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani katika ardhi ya Israel mwishoni mwa juma. Ikulu ya White House pia haikutoa maoni yoyote, lakini ripoti za vyombo vya habari zimesema Israel ilikuwa imeionya Washington mapema kuhusu mashambulizi hayo.

Safari za ndege zilisitishwa nchini Iran kutoka Tehran na miji mingine, kabla ya kuanza tena mapema asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.