Pata taarifa kuu

Israeli imerusha makombora kuelekea Iran kujibu shambulio dhidi yake

Israeli imerusha makombora nchini Iran kulipiza kisasi, baada ya kushambuliwa wiki iliyopita, kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa maafisa wa Marekani walionukuliwa na vituo vya Habari vya Marekani vya ABC, CBS na CNN. Israeli hajaizungumza chochote mpaka sasa.

Wanajeshi wa Israeli wakiwa katika oparesheni katika Ukanda wa Gaza katika vita dhidi ya Hamas. Novemba 8, 2023. REUTERS/Ronen Zvulun
Wanajeshi wa Israeli wakiwa katika oparesheni katika Ukanda wa Gaza katika vita dhidi ya Hamas. Novemba 8, 2023. REUTERS/Ronen Zvulun REUTERS - RONEN ZVULUN
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa kijeshi nchini Iran, wamesema wamefanikiwa kuangusha ndege tatu zisizokuwa na rubani kwa kutumia mitambo yake ya ulinzi wa anga katika mkoa wa Isfahan.

Hatua hii imesebabisha serikali ya Iran kusitisha safari za angaa kwenye baadhi ya miji.

Waandamanaji nchini Iran wakisherehekea shambulio la nchi yao dhidi ya Israeli mnamo Aprili 14, 2024 huko Tehran.
Waandamanaji nchini Iran wakisherehekea shambulio la nchi yao dhidi ya Israeli mnamo Aprili 14, 2024 huko Tehran. AFP - ATTA KENARE

Hatua hii inakuja baada ya Iran kurusha mamia ya makombora kulipiza kisasi dhidi ya Israeli wiki iliyopita, kulipiza kisasi kufuatia kitendo cha jeshi la Israeli kushambulia ubalozi wake jijini Damascus na kusababisha mauaji ya watu 13 wakiwa wakuu wake wa kijeshi.

Wiki hii, jumuiya ya Kimataifa ilitoa wito kwa Iran na Israeli kuepuka kuendeleza mzozo huu na kuonya kuwa iwapo utaendelea, usalama wa kikanda utakuwa mashakani.

Soma piaIran kujibu vikali iwapo Israeli italipiza kisasi shambulio la wikendi iliopita

Marekani ambayo ilikyuwa imeionya Israeli kuachana na mpango wowote wa kulipiza kisasi, haijazungumzia mashambulio haya.

Hillary Ingati- Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.