Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Marekani yadondosha misaada ya kibinadamu

Kwa mara ya kwanza, Marekani imefanya operesheni ya kudondosha misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza Jumamosi Machi 2. Kulingana na Umoja wa Mataifa, eneo hili la Palestina linatishiwa na njaa. Ndege tatu za kijeshi za Marekani zilidondosha "vifurushi" 66 sawa na zaidi ya milo 38,000.

Picha zilizorushwa na Wapalestina na jeshi la Jordan na Ufaransa zinawezesha kuelewa jinsi operesheni hiyo ilifanyika.
Picha zilizorushwa na Wapalestina na jeshi la Jordan na Ufaransa zinawezesha kuelewa jinsi operesheni hiyo ilifanyika. © Captures d'écran/ Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Nchi nyingine zimedondosha misaada ya kibinadamu katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Jordan, inayoungwa mkono na Ufaransa, Uholanzi na Uingereza. Misri, kwa ushirikiano na Falme za Kiarabu, pia imedondosha misaada ya kibinadamu. Kulingana na Kamati ya shirika lisilo la kiseikali la International Rescue Committee (IRC), "operesheni ya kudondosha misaada ya kibinadamu haiwezi na haipaswi kuchukua nafasi ya ufikiaji wa kibinadamu".

Siku ya Ijumaa, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza kwamba nchi yake itashiriki "katika siku zijazo" katika kudondosha misaada ya kibinadamu huko Gaza. 

"Tunaenda kusisitiza na kuiambia Israel kuwezesha kuingia kwa malori zaidi (...) Kwa kweli hakuna msaada wa kutosha unaowasili Gaza," Joe Biden amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.