Pata taarifa kuu

Gaza: Watu 30,320 wameuawa kulingana na ripoti mpya kutoka kwa Wizara ya Afya ya Hamas

Wizara ya Afya ya Hamas imetangaza Jumamosi Machi 2 idadi mpya ya watu 30,320 waliouawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina.

Mpalestina aliyejeruhiwa kwa risasi zilizofyatuliwa na wanajeshi wa Israel akisubiri kupata huduma, kwa mujibu wa mamlaka ya afya, amelala kitandani katika hospitali ya Al Shifa huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas katika mji wa Gaza, Machi 1, 2024.
Mpalestina aliyejeruhiwa kwa risasi zilizofyatuliwa na wanajeshi wa Israel akisubiri kupata huduma, kwa mujibu wa mamlaka ya afya, amelala kitandani katika hospitali ya Al Shifa huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas katika mji wa Gaza, Machi 1, 2024. © Kosay Al Nemer / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Pia imeripoti, katika taarifa yake, vifo 92 katika kipindi cha saa 24 zilizopita na jumla ya watu 71,533 waliojeruhiwa katika ardhi ya Palestina tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7.

Wakati huo huo Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat, ameituhumu Israeli kwa kile anachosema ni mauaji ya halaiki dhidi ya raia wa Palestina.

Faki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuanzisha uchunguzi baada ya watu waliokuwa wanataka kupewa chakula cha msaada kushambuliwa na Israeli.

Mamlaka huko Palestina inasema watu 100-waliuawa katika shambulio hilo wengine 750 wakiripotiwa kujeruhiwa.

Wanajeshi wa Israeli waliwafyatulia risasi raia wa Palestina siku ya Alhamis waliokuwa wanataka kupata sehemu ya chakula cha msaada.

Tukio lilitokea baada ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP kuonya kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa, huenda raia wa Kaskazini mwa Gaza wakakabiliwa na baa la njaa.

kwa upande mwngine Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatarajia kupatikana kwa muafaka wa kusitisha vita kati ya wapiganaji wa Hamas na Israeli kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kauli ya Biden imekuja wakati huu jamii ya kimataifa ikitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia hatua ya wanajeshi wa Israeli kutekeleza shambulio katika eneo la kutoa chakula cha msaada kwa raia wa Palestina kaskazini mwa mji wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.