Pata taarifa kuu

Israel yashambulia eneo la Bekaa, mashariki mwa Lebanon, ngome ya Hezbollah

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mapigano kwenye kati ya Lebanon na Israel, ndege za Israel zilmefanya mashambulizi karibu na mji wa Baalbeck, katika uwanda wa mashariki wa bonde la Bekaa. Mashambulio hayo yamesababisha vifo vya wapiganaji wawili wa Hezbollah.

Shambulio la anga kwenye viunga vya mji wa Baalbeck, ngome ya Hezbollah nchini Lebanon, Februari 26, 2024.
Shambulio la anga kwenye viunga vya mji wa Baalbeck, ngome ya Hezbollah nchini Lebanon, Februari 26, 2024. AP - STR
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Beirut, Paul Khalifeh

Maeneo yanayolengwa na jeshi la anga la Israel yapo karibu na mji wa Baalbeck, mojawapo ya ngome muhimu za Hezbollah inayojulikana kwa mahekalu yake ya Kirumi. Hii ni mara ya kwanza kwa ndege za Israeli kushambulia eneo hili, lililoko katika uwanda wa Bekaa, mashariki mwa Lebanon, kilomita 175 kutoka uwanja wa vita kati ya pande hizi mbili hasimu.

Vyanzo vya usalama na mashahidi wamesema mashambulio hayo yameharibu maghala ya kuhifadhia chakula, nyumba ya kukodi karibu na vituo hivi na gari. Ndege za Israel pia zimefanya mashambulizi dhidi ya ngome nyingine ya Hezbollah, Iqlim el-Touffah , mashariki mwa mji wa Saida, kilomita 55 kusini mwa Beirut.

Katika eneo hili, chama cha Hassan Nasrallah kimetangaza kuwa kiliidungua ndege isiyo na rubani ya Israel aina ya Hermès 450 mnamo Februari 26 kwa kutumia kombora la kutoka ardhini hadi angani. Video zinazoonyesha kifaa kikiwaka moto na mkondo wa moshi mweupe zimesambaa katika mitandao ya kijamii. Kisha ndege za Israel zimerusha makombora kwenye mabaki ya ndege hiyo isiyo na rubani.

Wakati huo huo, ubadilishanaji wa risasi na urushaji roketi kutoka eneo la mpakani kuelekea upade wa pili uliendelea, kama inavyofanywa kila siku tangu Oktoba 8, 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.