Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa unataka kukomesha mara moja mashambulizi kwenye Bahari Nyekundu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatoa wito kwa mataifa yote kuheshimu vikwazo vya silaha vinavyowalenga waasi wa wa Houthi kutoka Yemen. Azimio hilo lililotayarishwa na Marekani lakini pia Japan, limepitishwa kwa kura kumi na moja za kuunga mkono huku nchi nne zikikataa. Urusi, mwanachama wa kudumu, kwa hivyo haikutumia kura yake ya turufu. 

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatano hii, Januari 10, 2024 huko New York.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatano hii, Januari 10, 2024 huko New York. AFP - ANGELA WEISS
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio Jumatano jioni hii likitaka mataifa yote kuheshimu vikwazo vya silaha vinavyowalenga waasi wa Houthi wa Yemen, na kutaka kusitishwa "mara moja" kwa mashambulizi yao katika Bahari Nyekundu, "ambayo yanazuia biashara" na "kudhoofisha" haki na uhuru wa urambazaji", "amani" na "usalama wa eneo". Azmio hilo "linataka kwamba Wahouthi wasitishe mara moja" mashambulizi yao dhidi ya meli, "ambayo yanazuia biashara ya kimataifa na kudhoofisha haki na uhuru wa urambazaji, pamoja na amani na usalama wa ukanda huo".

■ Mkuu wa diplomasia ya Marekani alikutana na Mahmoud Abbas siku ya Jumatano mjini Ramallah hasa kushughulikia suala lenye utata la baada ya vita huko Gaza, eneo lililoharibiwa na mashambulizi ya Israel. Antony Blinken "alithibitisha tena kwamba Marekani inaunga mkono hatua zinazoonekana kuelekea kuundwa kwa taifa la Palestina." Kisha akasafiri kwenda Bahrain.

■ Mkuu wa diplomasia ya Marekani alikutana na Mahmoud Abbas siku ya Jumatano mjini Ramallah hasa kushughulikia suala lenye utata la baada ya vita huko Gaza, eneo lililoharibiwa na mashambulizi ya Israel. Antony Blinken "alithibitisha tena kwamba Marekani inaunga mkono hatua zinazoonekana kuelekea kuundwa kwa taifa la Palestina." Kisha akasafiri kwenda Bahrain.

■ Mashambulio ya anga ya Israel kusini na katikati mwa Ukanda wa Gaza yaliendelea siku ya Jumatano licha ya ahadi ya Israel ya kuelekea kwenye kampeni inayolengwa zaidi ya kuwahifadhi raia na kuwaondoa baadhi ya wanajeshi wake katika eneo la Palestina. Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina lilikumbwa na shambulio baya huko Deir el-Balah.

■ Kulingana na ripoti iliyotangazwa Jumatatu Januari 8 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 23,357 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu karibu 60,000 walijeruhiwa.

■ Kesi ya mauaji ya halaiki iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Ukanda wa Gaza inasikilizwa, leo Alhamisi, Januari 11, na pia Ijumaa, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko Hague (ICJ), nchini Uholanzi. Afrika Kusini iliwasilisha malalamiko yake mbele ya taasisi hii ya Haki ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita kuiomba kutoa uamuzi juu ya uwezekano wa vitendo vya "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.