Pata taarifa kuu

Baraza la Usalama laidhinisha azimio la kuboresha misaada ya kibinadamu kwa Gaza

Baada ya kuahirishwa mara kadhaa mfululizo, nakala ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitishwa huko New York. Maudhui yake yalikuwa mada ya mjadala mkali. Nakala mpya imerekebishwa kwa kiasi kikubwa chini ya uongozi wa Marekani, ambayo haikupiga kura, kama vile Shirikisho la Urusi.

Wawakilishi wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikutana mjini New York Ijumaa hii, Desemba 22, 2023 kupitisha azimio kuhusu misaada ya kibinadamu kwa Gaza.
Wawakilishi wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikutana mjini New York Ijumaa hii, Desemba 22, 2023 kupitisha azimio kuhusu misaada ya kibinadamu kwa Gaza. AP - Yuki Iwamura
Matangazo ya kibiashara

Azimio la kutaka msaada zaidi wa kibinadamu kwa Gaza limepitishwa huko New York, baada ya kuchelewa kwa wiki moja. Nakala "inahitaji pande zote kuidhinisha na kuwezesha uwasilishaji wa haraka, salama na usiozuiliwa wa msaada mkubwa wa kibinadamu", inataka "kuchukua hatua za haraka" katika suala hili na "kuunda mazingira ya kukomesha kwa kudumu kwa uhasama. Bila, hata hivyo, wito wa kusitisha mapigano mara moja, ambao Marekani haikutaka, kama linavyokumbusha shirika la habari la AFP.

Azimio hilo limeidhinishwa na nchi kumi na tatu. Hakuna mjumbe wa Baraza aliyepiga kura ya kupinga. Marekani na Urusi, wanachama wa kudumu wenye kura ya turufu, walijizuia.

Katika Baraza la Usalama, mjumbe wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour anasisitiza malengo matatu

Malengo haya ni kusitisha mapigano mara moja, misaada mikubwa ya kibinadamu na hakuna kulazimishwa kuhama. Bw. Mansour amekosoa vitendo vya Israeli huko Gaza mbele ya Baraza: "Tunachokabili," amesema, "ni jaribio la kuwaangamiza watu wetu na kuwaondoa milele kutoka kwa ardhi yao. Hili ndilo lengo la Israeli, hili ndilo lengo lake la kweli. Hakuna mustakabali wa Wapalestina huko Palestina. "Wapalestina wanakaribisha marekebisho yaliyopendekezwa na Urusi, lakini ambayo Marekani ilipiga kura ya turufu, na hata hivyo kueleza kuunga mkono azimio lililopitishwa, "hatua katika mwelekeo sahihi", kulingana na Bw. Mansour.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amejibu kuhusu kupitishwa huko New York kwa azimio la msaada wa kibinadamu kwa Gaza. Katika mtandao wa kijamii wa Xi, Eli Cohen amehakikisha kwamba nchi yake taendelea kuchukua hatua kwa kujibu, kulingana na sheria za kimataifa, lakini itapitia, kwa sababu za kiusalama, usaidizi wowote wa kibinadamu kwa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.