Pata taarifa kuu

Israel yaagiza watu kuhama Khan Yunis, jiji kubwa zaidi kusini mwa Gaza

Baada ya kuongezeka kwa operesheni huko Khan Younes, jeshi la Israel limeagiza kuhamishwa kwa sehemu ya watu katikamji huo mkubwa zaidi kusini mwa Gaza usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi.

Mtoto wa Kipalestina aliyejeruhiwa na mshambulio la anga la Israeli anapelekwa katika Hospitali ya Nasser iliyoko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 20, 2023.
Mtoto wa Kipalestina aliyejeruhiwa na mshambulio la anga la Israeli anapelekwa katika Hospitali ya Nasser iliyoko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 20, 2023. REUTERS - BASSAM MASOUD
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, watu 110,000 wanahusika na agizo hilo. Siku ya Jumatano, idadi ya watu waliouawa ilivuka 20,000 katika mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Israel yatangaza vifo vya wanajeshi watatu 

Jeshi la Israel limetangaza kuwa limepoteza wanajeshi wengine watatu, na kufikisha idadi ya wanajeshi 137 waliouawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini Oktoba 27 na 469 tangu mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba.

Mbali na vita huko Gaza, mzozo huo unaendelea kuchochea mvutano katika Mashariki ya Kati. Siku ya Alhamisi Hezbollah, mshirika wa Hamas nchini Lebanon, imetangaza kuwa imerusha maroketi kaskazini mwa Israel. Hapo awali, jeshi la Israel lilieleza kuwa lilishambulia "kituo cha kamandi" ya Hezbollah na kuwafyatulia risasi wapiganaji waliokuwa wakielekea mpakani karibu na Metula. Hezbollah imethibitisha kifo cha mpiganaji wake, aliyeuawa wakati "akielekea Jerusalem".

UNSC yashindwa kupitisha azimio kwa msimamo wa Marekani

Kwa kushindwa kupitisha azimio lake kwa msmmamo wa Marekani, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litajaribu tena siku ya Alhamisi kuzungumza kwa kali moja, wakati wa kura iliyoahirishwa mara kadhaa juu ya azimio lililokusudiwa kuongeza msaada kwa ukanda wa Gaza. Baraza hilo, ambalo limekosolewa vikali kwa kutochukua hatua tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, limekuwa likijadili nakala hii iliyoletwa na Falme za Kiarabu kwa siku kadhaa.

Kura iliokuwa imepangwa kufanyika Jumatatu iliahirishwa mara kadhaa, ya mwisho Jumatano kwa ombi la Marekani ambayo ilipiga kura ya turufu tarehe 8 Desemba dhidi ya nakala ya awali ikitaka "kusitishwa kwa mapigano" katika Ukanda wa Gaza. Diplomasia inachukua muda," alisema Lana Zaki Nusseibeh Balozi wa Falme za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano. Akiwa na matumaini ya matokeo "chanya" kutoka kwa mazungumzo haya ili kuvunja mkwamo, alihakikisha kwamba hata kama hali itakuwa sivyo, "kura itapigwa".

Tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, Baraza limeweza kuvunja ukimya wake mara moja tu, na azimio la Novemba 15 likitaka "kusitishwa kwa mapigano". Lilifutilia mbali nakala nyingine tano ndani ya miezi miwili, mbili kati yake zilitokana na kura za turufu za Marekani, ya mwisho mnamo Desemba 8.

Baadaye Marekani iliizuia, licha ya shinikizo kubwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Wanachama wengi wa Baraza wanaonekana kutaka kuepuka kura nyingine ya turufu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.