Pata taarifa kuu

Kura ya UNSC kuhusu usitishaji vita Gaza yaahirishwa hadi Jumanne

Kura ya Baraza la Usalama kuhusu hali ya Gaza, iliyopangwa Jumatatu, iliahirishwa hadi Jumanne ili kuruhusu mazungumzo juu ya nakala kuendelea, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.

Wanajeshi wa Israel wakiendesha operesheni zao katika Ukanda wa Gaza, Desemba 18, 2023.
Wanajeshi wa Israel wakiendesha operesheni zao katika Ukanda wa Gaza, Desemba 18, 2023. © Force de défense d'Israël / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Falme za Kiarabu, kwa asili ya rasimu mpya ya azimio ambalo linalenga kusitisha mapigano ili kuruhusu upatikanaji wa misaada ya kibinadamu, imeomba kuahirishwa kwa kura hiyo, ambayo inapaswa kufanyika Jumanne katika wakati ambao bado haujaamuliwa, vyanzo hivyo vimebainisha.

Wakati huo huo jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza, katika siku ya 72 ya vita. Baada ya milipuko mikali ya mabomu kwenye kambi ya Jabaliya, na katika hospitali kadhaa ikiwa ni pamoja na wodi ya wazazi ya hospitali ya Nasser huko Khan Younès, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipaswa kutoa uamuzi leo Jumanne , Desemba 19 kuhusu akala mpya ya kutaka " kusitishwa kwa dharura na mapigano” huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.