Pata taarifa kuu

Kuachiliwa kwa mateka: Serikali ya Israeli inakabiliwa na shinikizo

Wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana, leo Jumanne, Desemba 19, juu ya mswaada mpya unaotaka "kusitishwa kwa haraka na kwa kudumu kwa mapigano" katika Ukanda wa Gaza, serikali ya Israel pia inakabiliwa na shinikizo linaloongezeka ndani ya nchi kwa ajili ya mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka. 

Mabango yenye majina ya mateka Waisraeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza, yamebandikwa ukutani huko Tel Aviv, Israel, Novemba 22, 2023.
Mabango yenye majina ya mateka Waisraeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza, yamebandikwa ukutani huko Tel Aviv, Israel, Novemba 22, 2023. REUTERS - SHIR TOREM
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi miwili na nusu ya vita, Benjamin Netanyahu bado anasisitiza juu ya ulazima wa operesheni za kijeshi, lakini anajikuta akilazimika kufanya mazungumzo.

Waisraeli kadhaa walikusanyika Jumatatu, Desemba 18, mbele ya makao makuu ya Wizara ya Ulinzi na makao makuu ya jeshi huko Tel Aviv. Tangu shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7 nchini Israel, familia za mateka na watu waliopotea ndugu zao wameongeza hamasa zao kuiomba serikali kufanya kazi ili kurejesha wapendwa wao. Wamekuwa wakikusanyika katika eneo moja huko Tel Aviv, wakiandaa maandamano kila Jumamosi jioni, maandamano na mikutano mbele ya majengo ya serikali. Kauli mbiu yao ni: "Warudisheni nyumbani sasa".

Kwa jumla, watu 250, askari na raia, walikamatwa na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas. Kulingana na mamlaka ya Israel, 129 bado wanazuiliwa katika Ukanda wa Gaza. Picha za mateka hawa zinaonyeshwa kila mahali nchini Israeli: kwenye mabango, madaraja, kando ya barabara, lakini ndugu zao wanataka kuongeza shinikizo kwa serikali.

Shinikizo la kufikia makubaliano

Baada ya jeshi kutangaza tarehe 15 Desemba kwamba liliwaua kimakosa mateka watatu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ndugu wa mateka hao waliweka kambi mbele ya lango kuu la kuingilia Wizara ya Ulinzi. "Tunaomba kila mtu aje hapa haraka iwezekanavyo," Nadav Rudaeff alitangaza siku ya Jumatatu katika video iliyorushwa hewani na jukwaa la familia za mateka na watu waliopotea. “Tunawahitaji ninyi nyote na msaada wenu. Tutapiga kelele nyingi, tukiuliza na kutaka baraza la kivita liwasilishe makubaliano yatakayofikiwa kuwaachilia mateka wote. Tunataka kusikia kutoka kwao na si kutoka kwa mtu mwingine yeyote,” aliongeza, ambaye baba yake ni mateka katika Ukanda wa Gaza.

Siku ya Jumatatu jioni, waandamanaji walitembelewa na Gadi Eisenkot. Alama ya kuungwa mkono na mkuu wa zamani wa majeshi na mjumbe wa baraza la kivita, lakini pia kutoka kwa baba aliyefiwa: Mtoto wa Gadi Eisenkot aliuawa akiwa kazini huko Gaza mnamo Desemba 7. Kwa sasa, hata hivyo, familia za mateka hazijasikia uwasilishaji wa mpango wa kutolewa kwa wapendwa wao ambao wanasubiri.

Katika siku za hivi karibuni, serikali ya Israel ilibadili msimamo wake. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alithibitisha mnamo Desemba 16 kwamba alimwagiza mkuu wa Mossad - kitengo cha idara ya ujasusi kwa msuala ya nje ya nchi - kuanza tena mazungumzo na mpatanishi, ambaye ni Qatar. Mkutano ulifanyika Jumatatu hii huko Warsaw, Poland. Na kulingana na shirika la habari la Axios, ilikuwa mkutano wa pili kwa siku chache baada ya kwanza kufanyika siku ya Ijumaa jioni.

Tangu kumalizika kwa mapatano ya kwanza mnamo Desemba 1, mpatanishi wa Israeli na mpatanishi wa Qatar walikuwa hawajaonana tena. Hata hivyo, kwa mujibu wa shirika la habari la Axios, serikali ya Israel ilikuwa iliombwa na Qatar wiki moja kabla. Lakini baraza la kivita la Israel lilikataa pendekezo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.