Pata taarifa kuu

Gaza: Kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaahirishwa tena

Kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu azimio linalokusudiwa kuboresha hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza imeahirishwa tena hadi Ijumaa, duru kadhaa za kidiplomasia zimesema.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Oktoba 30, 2023 mjini New York.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Oktoba 30, 2023 mjini New York. © Michael M. Santiago / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kura ya azimio katika Umoja wa Mataifa imeahirishwa tena. Kwa upande wake rais wa Ufaransa yuko nchini Jordan akiwa na wanajeshi wa Ufaransa na kujaili na Mfalme wa nchi hiyo uwezkano wa kusitisha mapigano huko Gaza.

Wakati huo jeshi la Israel linaendelea na operesheni zake katika Ukanda wa Gaza, baada ya kuamuru kuhamishwa kwa mji wa Khan Younes siku ya Jumatano. Siku ya Jumatano, idadi ya waliouawa ilivuka kizingiti cha watu 20,000 katika mashambulizi ya Israel huko Gaza. Wakati jeshi la Israel linakadiria kuwa limewaua zaidi ya "magaidi" 2,000 tangu kumalizika kwa makubaliano ya Desemba 1.

Wito wa kusitishwa kwa mapigano unaendelea, hasa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza David Cameron anayezuru Misri. Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ameionya Israel juu ya hatari ya muda mrefu ya hatua zake za kijeshi huko Gaza.

Kwa upande mwingine Hamas imesema lengo la Israel la kuiangamiza "linaelekea kushindwa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.