Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: WHO yapitisha azimio la kutaka msaada wa haraka wa kibinadamu kwa Gaza

Jeshi la Israel na kundi la Hamas la Palestina wameendelea na mapigano makali Jumapili, Desemba 10 kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo mamia ya maelfu ya watu walijikuta wamekwama.

Kijana akishusha chakula kwenye lori kama sehemu ya misaada ya kibinadamu huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 10, 2023.
Kijana akishusha chakula kwenye lori kama sehemu ya misaada ya kibinadamu huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 10, 2023. AFP - MOHAMMED ABED
Matangazo ya kibiashara

Bodi ya Utendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imepitisha kwa makubaliano azimio la kutaka msaada wa haraka wa kibinadamu kwa Gaza. Wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa kupitisha azimio kuhusu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas, kutokana na kura ya turufu ya Marekani, nchi 34 wanachama wa Baraza la Utendaji la WHO zote zinataka "kupitishwa kwa haraka, endelevu na bila vikwazo misaada ya kibinadamu" katika Umoja wa Mataifa kwa Ukanda wa Gaza.

Hamas inasema hakuna mateka atakayeondoka Gaza "hai" bila "mazungumzo"

Hamas imeonya siku ya Jumapili kwamba hakuna mateka hata mmoja waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Oktoba 7 na ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza atakayeondoka "hai" bila mazungumzo na bila "kukidhi matakwa" yakundi hilo la wanamgambo la Palestina. "Wala adui wa kifashisti na uongozi wake wa kiburi, au wafuasi wake, wataweza kuwaokoa wafungwa wao wakiwa hai bila kufanya mazungumzo, na bila kukidhi matakwa ya Hamas," Abou Obeida, msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas amesema katika video.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.