Pata taarifa kuu

Benjamin Netanyahu: Vikosi vya Israel vimezingira nyumba ya kiongozi wa Hamas Gaza

Mapigano makali yanaendelea Alhamisi, Desemba 7, katika Ukanda wa Gaza kati ya Hamas na jeshi la Israel, ambalo liliuchukua mji mkubwa wa Khan Yunis ambapo inamsaka mtu inayemdhania kuwa ndiye aliyepanga shambulio la umwagaji damu Oktoba 7. 

Watu waliojeruhiwa katika milipuko ya mabomu katika Ukanda wa Gaza wanasafirishwa hadi hospitali ya Khan Younes, Ijumaa Desemba 1, 2023.
Watu waliojeruhiwa katika milipuko ya mabomu katika Ukanda wa Gaza wanasafirishwa hadi hospitali ya Khan Younes, Ijumaa Desemba 1, 2023. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

 

Katika jiji kikubwa zaidi kusini mwa Ukanda wa Gaza, askari wa kikosi cha ardhini cha Israeli, magari ya kivita na tingatinga yamewasili katikati mwa jiji, kulingana na mashahidi. Siku ya Jumatano jioni jeshi la Israel lilidai "kutoboa safu za ulinzi" za Hamas, "kuangamiza idadi fulani ya magaidi" na kuharibu karibu "lango 30 za mahandaki".

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vikosi vya Israel "vinazingira nyumba ya (Yahya) Sinwar," kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, huko Khan Yunis. "Sinwar anajificha chini ya ardhi," amesema Daniel Hagari, msemaji wa jeshi, akimaanisha mahandaki ya Hamas huko Gaza.

Usiku ulipoingia siku ya Jumatano, mawingu mazito ya moshi mweusi na miali ya moto viliendelea kuongezeka kutoka Gaza. Wakati wa mchana, njia zilizovutwa na roketi zilizorushwa kuelekea Israel kutoka Rafah, kusini mwa eneo dogo la Palestina, pia zilitanda angani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.