Pata taarifa kuu

RSF yatoa wito wa kufunguliwa kituo cha mpakani cha Rafah kwa waandishi wa habari

Shirika lisilo la kiserikali la Reporters Without Borders (RSF) linatoa wito siku ya Alhamisi kwa kivuko cha mpaka cha Rafah huko Gaza kufunguliwa kwa waandishi wa habari, ambapo jeshi la Israel limepanua operesheni zake za ardhini katika eneo lote. 

Karibu na mpaka na Misri, huko Rafah, Desemba 6, 2023.
Karibu na mpaka na Misri, huko Rafah, Desemba 6, 2023. REUTERS - SALEH SALEM
Matangazo ya kibiashara

Kivuko hiki kati ya Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, na Misri, kinadhibitiwa na Wapalestina na Wamisri. Hata hivyo, inasisitiza taarifa ya RSF kwa vyombo vya habari, "Israel inafuatilia shughuli zote kwenye mpaka wa kusini na ilipua lango hili la mpakani mara nne mwanzoni mwa vita".

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, shirika linatoa wito kwa mamlaka ya Israel na Misri "kufungua milango" ya kuvuka mpaka "ili waandishi wa habari waweze kuja na kwenda pande zote za mpakani". "Waandishi wa habari ambao walilazimika kuhama kaskazini sasa wameamriwa na Israeli kukusanyika kwenye mpaka na Misri, bila uwezekano wa kuvuka. Kinyume chake, waandishi wa kimataifa wanazuiwa kuingia,” shirika hilo linasisitiza.

"Katika kipindi cha miezi miwili ya vita, hakuna waandishi wa habari ambao wameruhusiwa kuingia Ukanda wa Gaza kupitia Rafah, ambayo inadhoofisha wazi uwezo wa vyombo vya habari kuripoti mzozo huo," RSF imeongeza katika taarifa. Na kukumbusha kwamba "waandishi wa habari 58 waliuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel huko Gaza, ikiwa ni pamoja na 14 wakati wa kazi zao".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.