Pata taarifa kuu

Kura ya Marekani katika Umoja wa Mataifa: Erdogan alaani "Baraza la Ulinzi la Israeli"

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameshutumu, Jumamosi, Desemba 9, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo amesema limekuwa "Baraza la Ulinzi la Israel," siku moja baada ya "kura ya turufu" ya Marekani kuhusu azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani kura ya turufu ya Marekani inayozuia azimio la baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usitishwaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani kura ya turufu ya Marekani inayozuia azimio la baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usitishwaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza. AP - Pavel Golovkin
Matangazo ya kibiashara

"Tangu Oktoba 7, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa baraza la ulinzi wa Israeli," ameshutumu rais wa Uturuki katika maadhimisho ya miaka 75 ya kutangazwa kwa haki za binadamu, linaripoti shirika la habari la AFP.

Kura ya turufu ya Marekani siku ya Ijumaa jioni katika Umoja wa Mataifa kuhusu azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano katika eneo la Palestina pia imelaaniwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, hususan shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), ambalo linataja kuwa Marekani wanahusika "katika njama ya mauaji makubwa katika Gaza. Huko Gaza, "watu wamekata tamaa, wana hofu na hasira," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilalamika siku ya Ijumaa, akitaja "mazingira mabaya ya kibinadamu."

Baada ya zaidi ya miezi miwili ya vita, zaidi ya nusu ya nyumba za Gaza zimeharibiwa au kuteketezwa katika eneo la Palestina, ambapo 85% ya watu wameyakimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. Kutokana na msongamano wa watu na hali duni ya usafi katika makao ya shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kusini mwa eneo hilo, baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kama vile kuhara, magonjwa ya kupumua yaliyokithiri na maambukizi ya ngozi yameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.