Pata taarifa kuu

Gaza: UNICEF ​​​​yaonya kuhusu 'janga la kibinadamu' ikiwa mapigano yataongezeka

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ameonya kuhusu "janga la kibinadamu" ikiwa mashambulizi ya Israel huko Gaza yataongezeka kwa kiwango kilichoshuhudiwa kabla ya usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na Hamas.

Wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza, Desemba 2, 2023.
Wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza, Desemba 2, 2023. via REUTERS - ISRAEL DEFENSE FORCES
Matangazo ya kibiashara

Catherine Russell pia amewataka "wahusika wote kuhakikisha kwamba watoto wanalindwa na kusaidiwa" na kutoa wito wa "kusitishwa kwa mapigano kwa ajali ya kutoa misaaada ya kibinadamu". 

Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF amesema katika taarifa yake kwamba Ukanda wa Gaza "kwa mara nyingine tena ni mahali hatari zaidi duniani kwa mtoto" na kwamba "watoto wengi zaidi bila shaka watapoteza maisha" kufuatia kuanza tena kwa mapigano.

Wizara ya afya ya Gaza inayodhibitiwa na kundi la wanamgambo la Hamas, imesema, karibu watu 240 wameuwawa Gaza tangu siku ya Ijumaa, baada ya kumalizika kwa muda wa siku saba wa kusitisha mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.