Pata taarifa kuu

Israel yafanya mashambulizi makali kwenye Ukanda wa Gaza, zaidi ya watu 200 wauawa ndani ya saa 24

Jeshi la Israel linashambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza Jumamosi hii, Desemba 2 kwa siku ya pili mfululizo tangu kumalizika kwa usitishwaji mapigano na Hamas, ambayo yaliwezesha kuachiliwa kwa mateka na kuwasilisha misaada ya dharura. Idadi ya vifo inaendelea kuongezeka, hasa katika eneo la Khan Younes.

Picha iliyopigwa kusini mwa Israeli, karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza, Desemba 2, 2023.
Picha iliyopigwa kusini mwa Israeli, karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza, Desemba 2, 2023. AFP - JACK GUEZ
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Makubaliano ya usitishwaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza yalivunjwa siku ya Ijumaa asubuhi, Desemba 1. Jeshi la Israel lilianza tena mashambulizi ya anga na Hamas ilianza tena kurusha roketi kuelekea Israel.

■ Idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imefikia zaidi ya watu 15,000 tangu kuanza kwa vita, wakiwemo watoto 6,150. Karibu watu 240 wameuawa tangu siku ya Ijumaa, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas, iliyoko madarakani katika eneo la Palestina. Tangu Oktoba 7, zaidi ya Waisraeli 1,200 wameuawa.

■ Wakati wa usitishwaji wa mapigano, mateka 110 - Waisraeli 86 na wageni 24 - waliachiliwa huru na Hamas, kulingana na hesabu ya Israeli. Kwa upande wake, Israel iliwaachia huru wafungwa 240 wa Kipalestina; Mateka 136 wanaendelea kushikiliwa huko Gaza, kwa mujibu wa jeshi la Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.