Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel limesema limeanza tena mapigano na Hamas huko Gaza.

Nairobi – Katika chapisho kwenye X, vikosi vya ulinzi vya Israeli vimesema kuwa Hamas walifyatua risasi kuelekea Israeli na hivyo kukiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Makubaliano ya hapo awali ya siku nne za usitishaji wa mapigano, yaliongezwa mara mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa
Makubaliano ya hapo awali ya siku nne za usitishaji wa mapigano, yaliongezwa mara mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

Haya yamejiri muda  mfupi kabla ya makubaliano ya usitishwaji vita kwa siku saba kukamilika, Israel imesema imeangusha roketi iliyorushwa kutoka Gaza huku vyombo vya habari vyenye uhusiano na kundi la Hamas vikiripoti milipuko na milio ya risasi kaskazini mwa Gaza.

Makubaliano ya hapo awali ya siku nne za usitishaji wa mapigano, yaliongezwa mara mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa.

Hadi kufikia Alhamisi, mateka 110 waliokuwa wameshikiliwa huko Gaza wameachiliwa huru tangu kuanza kwa mapatano hayo tarehe 24 Novemba, huku Israel ikiwa imewaachia huru wafungwa 240 wa Kipalestina.

Mashambulio ya Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7 yameripotiwa kusababisha vifo vya watu 1,200. Tangu wakati huo, wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas inasema zaidi ya watu 14,800 wameuawa katika kampeni ya kulipiza kisasi ya Israel, wakiwemo watoto wapatao 6,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.