Pata taarifa kuu

Israel-Hamas: Emmanuel Macron aelezea 'furaha yake' baada ya kuachiliwa kwa Mia Schem

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea 'furaha yake' baada ya kuachiliwa Alhamisi hii, Novemba 30, mateka wa Ufaransa mwenye asili ya Israel, Mia Schem, aliyekuwa mikononi mwa wanamgambo wa Hamas.

Mwanamume huyu akishikilia picha ya Mia Shem, mjini Tel Aviv, Oktoba 17, 2023.
Mwanamume huyu akishikilia picha ya Mia Shem, mjini Tel Aviv, Oktoba 17, 2023. AFP - GIL COHEN MAGEN
Matangazo ya kibiashara

"Ni furaha kubwa kwangu, kwa familia yake na kwa raia wote wa Ufaransa," ameandika rais wa Ufaransa kwenye X, zamani ikiitwa Twitter. "Mia Schem yuko huru", ameongeza.

"Pia ninaelezea mshikamano wangu na wale wote ambao wamesalia mateka wa Hamas. Ufaransa inashirikiana na washirika wake kupata kuachiliwa kwao haraka iwezekanavyo," ameandika Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Mia Shem, 21 aliyetekwa nyara wakati wa shambulio lililotekelezwa na Hamas Oktoba 7 kusini mwa Israel, alionekana Oktoba 16 katika video iliyorushwa hewani na kundi la wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina, akiwa amelala chini na kupokea matibabu kwenye mkono wake.

Mwanamke huyo alitekwa nyara kwenye tamasha la muziki la Tribe of Nova ambapo watu 364 waliuawa Oktoba 7 na wengine wengi kutekwa nyara na kupelekwa Ukanda wa Gaza. Kulingana na Jukwaa la Familia za Mateka au Waliopotea, Mia Shem, ambaye alikuwa akifanya kazi katika chumba cha kuchora tattoos, alikuwa kwenye tamasha hilo akiwa na rafiki yake, ambaye pia Mfaransa mwenye asili ya Israeli, Elya Toledano, 27, ambaye hatima yake haijulikani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.