Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Kundi la sita la mateka wa Israel waachiliwa huru

Usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na Hamas umeingia katika siku yake ya sita siku ya Jumatano. Wapatanishi wa kimataifa wanaongeza juhudi za kupata usitishaji vita wa kudumu. Mabadilishano mapya ya mateka wa Israel kwa wafungwa wa Kipalestina yanaendelea.

Msafara wa shirika la Msalaba Mwekundu uliobeba mateka wa Israel ukielekea Misri kutoka Ukanda wa Gaza huko Rafah, Jumatano, Novemba 29, 2023.
Msafara wa shirika la Msalaba Mwekundu uliobeba mateka wa Israel ukielekea Misri kutoka Ukanda wa Gaza huko Rafah, Jumatano, Novemba 29, 2023. AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

Raia kadhaa wa Israel waliokuwa mateka huko Gaza wameachiliwa Jumatano jioni kama sehemu ya makubaliano na Israel, vyombo vya habari vya Israel vinaripoti.

Wakati huo huo Rais wa Mamalaka ya Palestina Mahmoud Abbas ametoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa kimataifa ili kutatua mzozo wa Mashariki ya Kati. Mahmoud Abbas pia amesema Wapalestina wako tayari kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa kuhusu "mchakato mzito wa kisiasa" ambao utapelekea nchi huru katika Ukingo wa Magharibi, Gaza na Jerusalem Mashariki, maeneo yaliyotekwa na Israel wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967, limeripoti Gazeti la Haaretz, likinukuu shirika la habari la Associated Press.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.