Pata taarifa kuu

Yahya Sinouar, kiongozi wa kutisha wa Hamas Gaza, anayesakwa na Israeli

Kwa Waisraeli, yeye ni mtu aliyejihusisha na kuua: Yahya Sinouar, kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, anachukuliwa kuwa muandaaji na mhusika mkuu wa shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israeli. Akiwa na umri wa miaka 61, anajulikana sana na idara za ujasusi.

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas katika Ukanda wa Gaza, Yahya Sinwar, Aprili 30, 2022.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas katika Ukanda wa Gaza, Yahya Sinwar, Aprili 30, 2022. AP - Adel Hana
Matangazo ya kibiashara

“Ninamuota Sinouar, huwa naifikiria ninapokula… huwa naifikiria kila mara! », anakiri Michael Kobi. Akiwa na umri wa miaka 78, mkongwe huyu wa Shin Bet, ujasusi wa ndani wa Israeli, anasema hatakuwa na amani pindi Yahya Sinouar anakuwa bado hai, anasema mwandishi wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa. Alifanya kazi pamoja naye katika magereza ya Israel ambako alihusika na mahojiano. Alirekodi masaa 150 ya mahojiano na mtu ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa wanamgambo waliohusika na kuwasaka wahaini wa kadhia ya Palestina. “Sijawahi kumjua mtu katili hivyo,” anasema. Alitumia kisu cha nyama na kuwakata vichwa raia wa Israel. Huko Gaza, walimpa jina la utani, "mchinjaji wa Khan Yunis." Almeongea ukidhani amepigwa na baridi kali, ni mtu asiyejali. Hakuna kilichomgusa. "

"Mchinjaji wa Khan Younes"

Yahya Sinouar ni "uso wa uovu," msemaji wa jeshi la Israel alitangaza hivi karibuni. Alizaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Khan Younès huko Gaza, Yahya Sinouar alikulia katika kivuli cha Sheikh Yacine, mwanzilishi wa Hamas, anaripoti Murielle Paradon, mwandishi wa habari wa kitengo cha Kimataifa cha RFI. Hivi karibuni, alichukua uongozi wa wanamgambo waliopewa jukumu la kufuatilia na kuwasaka wasaliti. Ukatili wake unaedana na jina lake la utani alilopewa. Msimamo wake mkali  kwa Israeli unajulikana.

Michaël Kobi ambaye ni mzungumzaji mzuri wa Kiarabu, alizungumza naye, akijaribu kumelewa jinsi alivyo, maono yake. Akizuiliwa kwa muda wa miaka 22 jela nchini Israel, Yahya Sinouar alijifunza Kiebrania na alipata fursa ya kujifunza kuhusu adui, kabla ya kuachiliwa mwaka 2011 kama sehemu ya mazungumzo ya wafungwa yaliyolenga kumwachilia mwanajeshi Gilad Shalit, mikononi mwa Hamas. "Hakuwahi kuficha lengo lake," afisa huyo wa samani wa Idara ya ujasusi ya Israel anakumbuka.

Muandaaji na mhusika mkuu wa shambulio la Oktoba 7

Lakini alipokuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas huko Gaza mwaka 2017, hotuba yake ilibadilika. Yahya Sinouar anasema anataka kuendeleza kiuchumi eneo la Palestina badala ya kuanzisha vita. Je, ilikuwa mtazamo wake au nia ya dhati iliyoshindikana? Mtu huyu, mwenye haiba na ujanja, kwa vyovyote vile anashukiwa kuwa ndiye chimbuko la mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa ya Oktoba 7 ambayo yaliiingiza Israel katika hofu na kusababisha ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya Wagaza.

“Mwaka 1989, alisema alikuwa akipanga mauaji makubwa ya Wayahudi, kwa mujibu wa katiba ya Hamas. Kwa hivyo anazingatia kile alichofanya kuwa ni mafanikio. Tungelikuwa tayari tumewaangamiza tangu kitambo. "

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant aliapa "kumpata" na "kumuangamiza". Anashukiwa kuwa anajificha kwenye mahandaki huko Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.