Pata taarifa kuu

Usitishwaji vita Gaza: Wapatanishi wanafanya kinachowezekana kujaribu kurefusha muda

Usitishwaji wa wamapigano kati ya Israel na Hamas unaingia siku yake ya sita Jumatano hii kwa zoezi jipya la kubadilishana mateka wa Israel na wafungwa palestina, wakati wapatanishi wa kimataifa wakiongeza juhudi za kupata usitishaji vita wa kudumu.

Wananchi wa Gaza wakitafakari ukubwa wa uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israel, huko Khan Younes, Novemba 29, 2023.
Wananchi wa Gaza wakitafakari ukubwa wa uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israel, huko Khan Younes, Novemba 29, 2023. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

Chanzo kilicho karibu na Hamas kimeliambia shirika la habari la AFP Jumatano hii kwamba kundi hilo "limekubali kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa siku nne" huku makubaliano ya kubadilishana kati ya mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina yanatarajiwa kukamilika Alhamisi asubuhi. "Hamas ina uwezo wa kuwaachilia wafungwa wa Israel inaowashikilia na makundi mengine yanayopamabana katika kipindi hiki, chini ya makubaliano ya sasa na kwa masharti sawa," chanzo hiki kimesema.

Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, majeshi ya Israel yaliwashauri Wapalestina dhidi ya kusafiri hadi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, licha ya kuwepo na kurefushwa kwa mapatano hayo. "Msijaribu kwenda kaskazini mwa Gaza, eneo ambalo linachukuliwa kuwa la kivita. Mnaweza tu kwenda kusini mwa Wadi Gaza kupitia barabara ya Salah al-Dine,” imeandikwa. “Ni marufuku kukaribia chini ya kilomita moja kutoka mpakani. Kuingia baharini ni marufuku. "

Wakati hu jeshi la Israel limeutangaza mji wa Jenin kuwa eneo lililofungwa la kijeshi, kutokana na mapigano yanayoendelea katika eneo hilo kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Kipalestina.

Duru za ndani zimesema kuwa wanajeshi wa Israel walivamia mji huo uliopo katika eneo lililokaliwa kwa mabavu na Israeli la Ukingo wa Magharibi na kuzingira nyumba moja, huku watu wakiukimbia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.