Pata taarifa kuu

Hamas inataka kuongezwa muda wa usitishaji wa vita

Nairobi – Wakati huu muafaka wa uisitishaji vita kati ya Hamas na Israel ukiendelea kwa siku mbili zaidi, chanzo kilichokaribu na kundi la Hamas kinasema upande huo uko tayari kuongeza muda huo kwa siku nne zaidi.

Vyanzo vya karibu na Hamas vinasema wanalenga kuongeza muda huo ilikutoa nafasi ya kubadilishana mateka na wafungwa
Vyanzo vya karibu na Hamas vinasema wanalenga kuongeza muda huo ilikutoa nafasi ya kubadilishana mateka na wafungwa AP - Mohammed Hajjar
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kundi hilo linalenga kutumia muda huo kuwaachia huru mateka zaidi wa Israeli kwa kubadilishana na wafungwa wa Palestina wanaozuiliwa na Tel Aviv.

Haya yanajiri wakati huu wapatanishi wa mzozo huo wakiendelea kutafuta suluhu la kudumu kumaliza mapigano ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya raia kwenye eneo la Gaza.

Tayari mateka 60 wa Israeli wameachiwa huru kwa mujibu wa makubaliano ya sasa wakati raia 180 wa Palestina wameachiwa, wakiwemo raia wa kigeni, wengine wakitarajiwa kuachiwa huru hii leo.

Licha ya usisitishaji wa muda wa vita, waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netenyahu, mapema wiki hii alisema kuwa hatua hiyo haimaanishi mapigano yamekamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.