Pata taarifa kuu

Paris na Berlin zakaribisha kuachiliwa kwa mateka na kutekelezwa kwa usiishaji mapigano

Ufaransa imekaribisha kuachiliwa kwa kundi la kwanza la mateka 24 walioachiliwa huru na Hamas na kuanza kutekelezwa kwa usitishaji wa mapigano huko Gaza kama sehemu ya makubaliano kati ya Israel na kundi la wapiganaji la Hamas kutoka Palestina. 

Gari la usafiri la gereza la Israeli linasafirisha wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa na mamlaka ya Israeli kutoka gereza la kijeshi la Ofer karibu na Jerusalem, Ijumaa, Novemba 24, 2023.
Gari la usafiri la gereza la Israeli linasafirisha wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa na mamlaka ya Israeli kutoka gereza la kijeshi la Ofer karibu na Jerusalem, Ijumaa, Novemba 24, 2023. AP - Mahmoud Illean
Matangazo ya kibiashara

Paris bado "imehamasishwa kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka wa Ufaransa ndani ya mfumo wa makubaliano yanayotekelezwa sasa", kuachiliwa kwa"wananchi wetu wote (kuwa) kipaumbele kabisa kwa Ufaransa, na tunafanya kazi bila kuchoka kuhakikisha wanaachilia mateka wote", Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema katika taarifa. 

Ufaransa pia imekaribisha "juhudi za upatanishi za Qatar, Misri na Marekani, na pia shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu, ambalo limefanya iwezekane kupata makubaliano haya. 

Ujerumani pia imekaribisha kuachiliwa kwa mateka wa kwanza, ikiwa ni pamoja na raia wanne wenye uraia pacha( Ujerumani na Israeli).

 "Nimefarijika sana kwamba mateka 24 wameachiliwa hivi punde huko Gaza, wakiwemo Wajerumani wanne, na kwamba baba, baada ya siku 49 akishikiliwa mateka na kuinilwa hofu nyingi hatimaye anaweza kuwakumbatia binti zake wawili wadogo na mke wake," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.