Pata taarifa kuu

Usitishaji vita kuanza kutekelezwa Ijumaa katika Ukanda wa Gaza

Usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas utaanza kutekelezwa huko Ukanda wa Gaza mapema Ijumaa asubuhi na kundi la kwanza la mateka 13 wataachiliwa alasiri, Qatar imetangaza siku ya Alhamisi, huku Hamas ikithibitisha mabadilishano hayo na wafungwa wa Kipalestina.

Mabango yenye majina ya mateka wa Israeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza, yakiwa yamebandikwa ukutani huko Tel Aviv, Israel, Novemba 22, 2023.
Mabango yenye majina ya mateka wa Israeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza, yakiwa yamebandikwa ukutani huko Tel Aviv, Israel, Novemba 22, 2023. REUTERS - SHIR TOREM
Matangazo ya kibiashara

"Usitishaji wa mapigano utaanza kutekelezwa saa 7:00 asubuhi saa za Mashariki ya Kati siku ya Ijumaa," amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Majed Al-Ansari, akibaini kwamba mateka 13 wa kike na watoto wataachiliwa "karibu saa kumi alaasiri, siku hiyo hiyo”, wakati mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza yakiendelea siku ya Alhamisi.

Tawi lenye silaha la kundi la Hamas limethibitisha kuanza kwa makubaliano hayo saa 7:00 asubuhi ya siku ya Ijumaa, na "kusitishwa kabisa kwa shughuli za kijeshi" kwa siku nne, ambapo mateka 50, wanawake na watoto chini ya miaka 19, wataachiliwa na wakati huo huo wafungwa watatu wa Kipalestina, wanawake na watoto wataachiliwa pia kutoka mikononi mwa mamlaka nchini Israel".

Israel imethibitisha Alhamisi kwamba "imepokea orodha ya kwanza ya majina" ya mateka, na ikasema "imewasiliana na familia zote." Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu haikubainisha iwapo inazungumzia mateka wote, wote watakaoachiliwa huru au kundi la kwanza husika.

Siku ya Jumatano Qatar, mpatanishi mkuu, alitangaza, siku ya 47 ya vita, kusitisha mapigano kwa siku nne, kutoa nafasi ya kubadilishana mateka wanaoshikiliwa Gaza na Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela tatu za Israel.

Makubaliano hayo yanatoa nafasi ya kubadilishana "mateka 10 kwa wafungwa 30" katika siku ya kwanza ya mapatano hayo, kwa jumla ya mateka 50 wa kiraia watakaoachiliwa huru katika siku nne kwa Wapalestina 150. Israel imetoa orodha ya wafungwa 300 ambao huenda wakaachiliwa, wakiwemo wanawake 33 na vijana 267 walio chini ya umri wa miaka 19.

Siku ya Jumatano, jumuiya ya kimataifa ilikaribisha makubaliano hayo, kwa kuyaona kuwa ni hatua ya kwanza kuelekea usitishaji vita wa kudumu. Makubaliano haya "hayawezi tu kuwa ya muda", hata hivyo, ameonya balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, akitaka itumike kuzuia "kuanza tena kwa uchokozi" wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.