Pata taarifa kuu

Israel: Hakuna suluhu katika mapigano au kuachiliwa kwa mateka kabla ya Ijumaa

Tzachi Hanegbi, mkuu wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Israel amesema katika taarifa yake kuwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza hawataachiliwa huru hadi Ijumaa.

Ndugu wa mateka wa Israel walioshikiliwa huko Gaza, Tel Aviv, Novemba 22, 2023.
Ndugu wa mateka wa Israel walioshikiliwa huko Gaza, Tel Aviv, Novemba 22, 2023. AFP - AHMAD GHARABLI
Matangazo ya kibiashara

Hakuna mateka wa Israel anayeshikiliwa na Hamas atakayeachiliwa kabla ya Ijumaa, alitangaza mkuu wa Baraza la Usalama la Taifa la Israel, Tzachi Hanegbi, wakati makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa kundi la kwanza la mateka viikuwa vikikitarajiwa leo Alhamisi.

"Mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka wetu yanaendelea bila shaka." Zoezi hili la kuachiliwa kwa mateka litaanza "siku ya Ijumaa", amesema usiku katika taarifa, bila kutoa maelezo.

Hakutakuwa na maelewano katika mapigano kati ya Israel na kundi la wapiganaji la Hamas kutoka Palestina kabla ya Ijumaa, kinyume na wahusika wakuu walivyotangaza awali, afisa wa Israel pia ameliambia shirika la habari la AFP.

Angalau mateka 50 kuachiliwa katika siku zijazo?

Vyombo vya habari vya Israel viliripoti mpango wa kuwaachilia mateka wa kwanza saa sita mchana. Ofisi ya serikali ilialika waandishi wa habari Tel Aviv mwishoni mwa jioni kwenye kituo cha waandishi wa habari kilichopewa jina la "kurejea kwa mateka".

Serikali ya Israel ilibaini kwamba iliidhinisha makubaliano haya ambayo yanahusu kuachiliwa kwa mateka wasiopungua 50, wanawake na watoto, ikitaja kuwa kwa upande wake "watasitisha mapigano" kwa siku nne. Kulingana na serikali ya Israel, mateka 50 wataachiliwa huru kwa kubadilishana na wafungwa 150 wa Kipalestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.