Pata taarifa kuu

Waasi nchini Yemen wadai kuwa wamerusha ndege zisizo na rubani kuelekea Israel

Waasi wa Houthi nchini Yemen wamesema Jumanne kuwa wamerusha ndege zisizo na rubani kuelekea Israel, kujibu vita vya nchi hiyo dhidi ya Hamas. 

Waasi wa Houthi wanadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Yemen na mji mkuu Sanaa.
Waasi wa Houthi wanadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Yemen na mji mkuu Sanaa. AP - Hani Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israel hapo awali lilidai kuwa liligundua "ndege sio narubani" kwenye mji wa Bahari Nyekundu wa Eilat. Akihojiwa na AFP, Waziri Mkuu wa serikali ya Houthi, Abdelaziz ben Habtour, amethibitisha kuwa "ndege hizi zisizo na rubani ni za Yemen".

Wakati huo huo wizara ya Afya (Hamas) imetangaza kuwa watu 8,525 wamefariki katika operesheni za Israeli katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7. Miongoni mwa wahanga hao, watoto 3,542 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita vya Israel. Kulingana na wizara, wanawake 2187 wameuawa katika vita hivyo. Eneo la Palestina bado limefungwa kwa vyombo vya habari vya kigeni kutoka Israel au Misri.

Siku ya JumatatuWaziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu alifutilia mbali usitishaji vita wowote katika vita dhidi ya Hamas, ingawa ilitakwa na mashirika ya kibinadamu ambayo yanachukizwa na hali mbaya katika ardhi ya Palestina.

Nchini Uingereza, Paul Bristow, mbunge wa kihafidhina na msaidizi wa waziri katika Idara ya Sayansi, Ubunifu na Teknolojia, amefukuzwa kwenye wadhifa wake baada ya kumtaka Rishi Sunak kuunga mkono usitishaji vita huko Gaza.

Watu 240 ndio wanashikiliwa mateka na Hamas kwa mujibu wa jeshi la Israel

Wakati wa taarifa yake ya asubuhi kwa vyombo vya habari leo Jumanne, msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema "watu 240 wametekwa nyara" na kushikiliwa mateka na Hamas. "Idadi hii imeongezeka kwa sababu baadhi ya mateka sio raia wa Israeli, kwa hivyo mchakato wa utambuzi ni mgumu zaidi," amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.