Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel latangaza kuachiliwa kwa mwanajeshi aliyetekwa na Hamas

Jeshi la Israel limetangaza kuwa limemkomboa mwanajeshi aliyekuwa ameshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas katika Ukanda wa Gaza, mamlaka ya Israel imesema. 

Picha iliyopigwa kutoka upande wa Israeli wa mpaka na Ukanda wa Gaza, Oktoba 30, 2023, inaonyesha moshi ukifuka wakati wa mashambulizi ya Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas.
Picha iliyopigwa kutoka upande wa Israeli wa mpaka na Ukanda wa Gaza, Oktoba 30, 2023, inaonyesha moshi ukifuka wakati wa mashambulizi ya Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas. © Ménahem Kahana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu "askari Ori Megidish amekombolewa, wakati wa operesheni ya ardhini, baada ya kutekwa nyara na kundi la kigaidi la Hamas mnamo Oktoba 7," iimebainisha idara ya usalama wa ndani na jeshi la Israeli katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari.

Mapigano makali yanaripotiwa huko Gaza kati ya jeshi la Israel na Hamas. Operesheni ya ardhini inaendelea katika eneo la Palestina. Mapema siku ya Jumatatu, Hamas pia ilitoa video inayoonyesha wanawake watatu wakionyeshwa kama mateka, kulingana na mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema jeshi la Israel limekuwa likisonga mbele "kimbinu" katika Ukanda wa Gaza katika siku ya 24 ya vita kati ya Israel na Hamas. "IDF imepanua uingiaji wake wa ardhi katika Ukanda wa Gaza, inafanya hivyo katika hatua zilizopimwa na zenye nguvu sana, ikiendelea kwa utaratibu hatua kwa hatua," amesema katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la mawaziri.

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema siku ya Jumatatu kwamba kifo cha mwanamke mwenye urai pacha (Ujerumani na Israel) Shani Louk kimeonyesha kile alichokiita ukatili wa Hamas na haja ya kuwajibisha kundi la wanamgambo wa Kipalestina. Serikali ya Israel imethibitisha siku ya Jumatatu kifo cha mwanamke huyu mwenye urai pacha, ambaye alitekwa nyara na Hamas wakati wa tamasha la muziki Oktoba 7 wakati wa shambulio baya lililoua watu 1,400, wengi wao wakiwa raia wa kawaida. "Kwangu mimi habari hii ni mbaya," Scholz alisema wakati wa ziara ya kiserikali barani Afrika. "Hii inaonyesha ukatili unaofanywa na Hamas. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.