Pata taarifa kuu

Syria: Marekani yafanya mashambulio ya anga dhidi ya ngome za Iran

Marekani imefanya mashambulizi Alhamisi Oktoba 26 dhidi ya vituo viwili vinavyotumiwa na kikosi cha walinzi wa Mapinduzi ya Iran na "makundi washirika" mashariki mwa Syria, ametangaza Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.

Ndege za Marekani zililenga kambi ya mafunzo ya wanamgambo wanaoiunga mkono Iran karibu na mji wa Mayadeen kusini mwa mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor, karibu na mpaka wa Syria na Iraq.
Ndege za Marekani zililenga kambi ya mafunzo ya wanamgambo wanaoiunga mkono Iran karibu na mji wa Mayadeen kusini mwa mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor, karibu na mpaka wa Syria na Iraq. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Beirut, Paul Khalifeh

Mkuu wa Pentagon amebaini kwamba mashambulizi haya yanayoelezwa kama "kujilinda na usahihi ni jibu kwa mfululizo wa mashambulizi yanayoendelea, na mengi yaliyofeli, dhidi ya wafanyakazi wa Marekani nchini Iraq na Syria na wanamgambo wanaoungwa mkono na 'Iran'. Mashambulizi haya yamesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 21 kujeruhiwa kidogo tangu Oktoba 17.

Ndege za Marekani zililenga kambi ya mafunzo ya wanamgambo wanaoiunga mkono Iran karibu na mji wa Mayadeen kusini mwa mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor, karibu na mpaka wa Syria na Iraq.

Ndege nyingine zilishambulia eneo la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran kaskazini zaidi, katika mkoa huo huo.

Vikosi vya Tehran na wanamgambo wake wasaidizi wa utaifa wa Syria, Iraq na Afghanistan wamewekwa katika maeneo haya kwa miaka kadhaa.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria limeripoti mashambulizi manne ambayo yalilenga ngome za Iran na washirika. Magari ya kubebea wagonjwa yaliwahamisha waathiriwa na kuwapeleka katika hospitali katika mji wa mpakani wa Boukamal, unaochukuliwa kuwa makao makuu ya kikosi cha walinzi wa Mapinduzi ya Iran nchini Syria.

Mashambulizi haya ya anga yanakuja baada ya kuongezeka kwa mashambulizi yanayodaiwa na "Upinzani wa Kiislamu nchini Iraq" dhidi ya ngome za Marekani nchini Syria na Iraq tangu kuanza kwa mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.

Nchini Syria, kambi ya Marekani katika kisima cha mafuta cha Conico huko Deir Ezzor imekuwa ikilengwa mara kwa mara na roketi na ndege zisizo na rubani.

Shirika la Kuchunguza Haki za Kibinadamu la Syria liliripoti kuwa ndege kubwa ya Marekani ilitua kwenye kambi hiyo siku ya Alhamisi ili kuwahamisha watu waliojeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.