Pata taarifa kuu

Baada ya ziara yake nchini Israel, Macron azuru Misri

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaendelea na ziara yake mjini Cairo siku ya Jumatano yenye lengo la kuzuia ongezeko la mapigano baada ya shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba na kuzindua upya "mchakato wa amani" wa kuundwa kwa taifa la Palestina.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi wakati wa mkutano wao huko Cairo Oktoba 25, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi wakati wa mkutano wao huko Cairo Oktoba 25, 2023. AP - Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutua kwa mara ya kwanza Jumanne nchini Israel, ambapo aliwasilisha salamu za rambirambi za "nchi rafiki, inayoomboleza mbele ya kitendo kibaya zaidi cha kigaidi katika historia yako", mkuu wa nchi anataka kukutana na viongozi wa Kiarabu katika ukanda huo.

Baada ya kukutana asubuhi huko Amman na Mfalme Abdullah II wa Jordan, atakutana Cairo na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi. 

Misri ni mpatanishi muhimu kati ya Palestina na Israeli na ni sehemu ya mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka zaidi ya 200 waliotekwa nyara nchini Israel na Hamas. 

Ni kutoka Misri ambapo lori za misaada ya kibinadamu zimekuwa zikiwasili hatua kwa hatua tangu Jumamosi, kwa usimamizi wa Umoja wa Mataifa, ambao unatoa wito wa msaada mkubwa kwa Wagaza milioni 2.4 walionyimwa kila kitu.

Huko Jordan, Emmanuel Macron pia alijadili hali hiyo na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA). "Upatikanaji wa umeme hasa kwa hospitali, upatikanaji wa maji na msaada wa chakula: tunatakiwa kujibu mahitaji ya haraka ya Wapalestina," amebaini kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) akitoa akipongeza shirika hilo "ambalo jukumu lake kwa raia ni muhimu”.

Bwana Macron pia alimtembelea rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu siku ya Jumanne ili kuonyesha uungaji wake mkono kwa raia wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.