Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron nchini Israel kutoa wito wa kuanzishwa upya kwa mchakato wa amani

Emmanuel Macron amewasili nchini Israel Jumanne hii, Oktoba 24, akiwa na nia ya kufanyia kazi usitishaji vita na kujaribu kupaza sauti ili Ufaransa isikike, kwa kuomba suluhu ya mataifa mawili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipeana mkono na rais wa Israel Isaac Herzog wakati wa mkutano mjini Jerusalem, Oktoba 24, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipeana mkono na rais wa Israel Isaac Herzog wakati wa mkutano mjini Jerusalem, Oktoba 24, 2023. AFP - CHRISTOPHE ENA
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea "uungaji mkono" wa Ufaransa kwa Israeli na Wafaransa huko Israeli na kupendekeza kuanzishwa tena "mchakato wa kweli wa amani" baada ya shambulio baya la Hamas mnamo Oktoba 7. 

Emmanuel Macron amekuwa akibaini kwamba atafanya ziara nchini Israel ikiwa safari kama hiyo inaweza kuwa "muhimu" kwa ukanda mzima wa Mashariki ya Kati. Wakati huu umewadia kulingana na Ikulu ya Élysée.

Malengo kadhaa, kipaumbele kimoja

Emmanuel Macron yuko nchini Israel akiwa na malengo kadhaa, anaelezea Valérie Gas, mwandishi wa habari wa RFI, katika kitengo cha siasa. Lengo la kwanza: kutoa ujumbe wa "mshikamano kamili" kwa Waisraeli na kwa waathiriwa wa shambulio la Hamas, ambapo atakutana na familia zao. Sharti muhimu kutoka kwa mtazamo wa Élysée. Pia, Mkuu wa Nchi ana nia ya kuweka mapendekezo ya "utendaji" mezani ili kukomesha mmizozo katika kanda hiyo na kufungua mtazamo wa kisiasa kwa ajili ya amani.

Kwa mujibu wa Paris, hatua hii ya mwishoinaendana sambamba na kuundwa kwa taifa la Palestina. Emmanuel Macron anakusudia kufichua matamanio haya kwa mamlaka ya Israeli na viongozi wa nchi za ukanda huo, kwa matumaini ya "kuruhusu kupita kwa misaada ya kiraia". Lakini juu ya yote - na hiki ndicho kipaumbele cha rais wa Ufaransa - atajaribu kuwaondoa mateka ambao bado wanashikiliwa huko Gaza na Hamas. Takriban raia 30 wa Ufaransa waliuawa katika shambulizi la Hamas, idadi kubwa zaidi ya vifo tangu shambulio la Julai 14, 2016 huko Nice kusini mwa Ufaransa. Wengine saba hawajulikani walipo, ikiwa ni pamoja na mateka salama na wengine kadhaa ambao huenda wanashikiliwa na Hamas huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.