Pata taarifa kuu

Idadi ya waliofariki Gaza yafikia 5,000, karibu nusu yao wakiwa watoto

Wanajeshi wa Israeli wameendeleza kutekeleza mashambulio ya angaa dhidi ya Wapalestina, wakati huu Wizara ya afya katika ukanda wa Gaza ikisema, watu zaidi ya 400 wameuawa kwa kipindi cha saa 24 zilizopita kwenye eneo hilo.

Wapalestina wakihamishwa kutoka kwa majengo baada ya mashambulizi ya Israel huko Deir al-Balah, Ukanda wa Gaza, Oktoba 22, 2023.
Wapalestina wakihamishwa kutoka kwa majengo baada ya mashambulizi ya Israel huko Deir al-Balah, Ukanda wa Gaza, Oktoba 22, 2023. © Hatem Moussa / AP
Matangazo ya kibiashara

Israel inasema, inalenga miundombinu ya Hamas katika mashambulio yanayoendelea, ikisema huenda vita vinavyoendelea vikaendelea kwa miezi kadhaa.

Aidha, jeshi la Israeli linasema, limetekeleza mashambulio yaliyopimwa, ili kupata taarifa muhimu kuhusu walikomateka waliochukuliwa na Hamas.

Licha ya Israeli kuwaambia Wapalestina, kuhamia Kusini mwa Gaza, Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi wa Kipalestina inasema, hali eneo la Kusini ni mbaya na raia wa kawaida hawana pa kwenda.

Katika hatua nyingine, kundi la Hamas limesema limetekeleza mashambulio mawili kwenye kambi za jeshi la Israeli. Jeshi la Israeli linasema limezuia mashambulio hayo.

Kesho rais wa Ufaransa atazuru jijini Tel Aviv kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Vita vinavyoendelea vimesababisha vifo vya Waisraeli 1,400, huku Wapalestina zaidi ya 5,000 wakiuwa na makaazi yao kuharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.