Pata taarifa kuu

Israel-Hamas: Macron kukutana na viongozi wa vyama kujadili hatari ya mvutano nchini Ufaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amechukua hatua Alhamisi baada ya shambulio lisilokuwa la kawaida la Hamas nchini Israeli, kutafuta "umoja wa taifa" katika kukabiliana na migawanyiko ya kisiasa na hatari ya kuingizwa kwa mzozo nchini Ufaransa. Mkutano na viongozi wa chama, ulifuatiwa na hotuba nzito.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awaleta pamoja viongozi wa kisiasa kwa minajili ya ujenzi wa taifa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awaleta pamoja viongozi wa kisiasa kwa minajili ya ujenzi wa taifa. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Nchi, akiambatana na Waziri Mkuu Elisabeth Borne, aliwaalika siku ya Jumatano saa sita mchana katika ikulu ya Elysée viongozi wa vyama 11 vinavyowakilishwa bungeni, pamoja na marais wa Seneti, Bunge la kitaifa na Baraza la Uchumi, Kijamii na Mazingira.

Katika kikako hiki wamejadili hali inayojiri nchini Ufaransa "kufuatia vitendo vya kigaidi vilivyofanywa nchini Israeli". Baadaye, rais wa Ufaransa atahutubia wananchi wa Ufaransa saa mbili kamili usiku.

Idadi ya watu waliouawa kutokana na shambulio hilo lililozinduliwa siku ya Jumamosi na vuguvugu la wapiganaji wa Kiislamu wa Palestina katika jimbo la Kiyahudi inazidi watu 1,200, huku jibu la Israel katika Ukanda wa Gaza likiwaua zaidi ya watu 1,000.

Takriban watu 11, raia wa Ufaransa waliuawa katika shambulio hilo na wengine 18 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto kadhaa "pengine waliotekwa nyara" na Hamas, kulingana na serikali.

"Kutokana na vitendo hivi vya kigaidi ambavyo Wafaransa wamekuwa wahanga", rais anataka "kuchunguza hali hii" na "kukusanya maoni ya viongozi wa chama" katika mfumo "unaojenga", anasema mmoja wa washauri wa rais. Kikao ambacho kitafanyika kwa faragha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.