Pata taarifa kuu

Misri iliitahadharisha Israel 'siku tatu' kabla ya shambulio la Hamas

Misri iliitahadharisha Israel juu ya hatari ya kutokea kwa ghasia "siku tatu" kabla ya shambulio la Hamas, amesema mbunge wa Marekani Michael McCaul, mkuu wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Baraza la Wawakilishi, siku ya Jumatano

Shambulio la Hamas nchini Israel limesababisha mamia ya watu kupoteza maisha.
Shambulio la Hamas nchini Israel limesababisha mamia ya watu kupoteza maisha. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Tunajua kwamba Misri iliwaonya Waisraeli siku tatu kabla kwamba tukio kama hilo linaweza kutokea," amesema baada ya taarifa kwa Bunge la Marekani. "Onyo lilitolewa, swali ni kujuwa ni katika ngazi gani," amesisitiza.

Misri haijawahi kutoa rasmi maoni yoyote juu ya habari hii, iliyotolewa kwenye vyombo vya habari siku kadhaa zilizopita. Lakini, kwa mara ya pili tangu kuanza kwa vita, siku ya Jumatano, "vyanzo vilivyowekwa sana katika vyombo vya usalama vya Misri" vilivyotajwa na vyombo vya habari vilivyo karibu na idara ya kijasusi ya Misri "vimekanusha ripoti za vyombo vya habari vya Israeli kuthibitisha kwamba idara za ujasusi za Misri ziliijulisha mamlaka ya Israelkuhusu nia ya Hamas kufanya shambulio hilo lililotokea tarehe Oktoba 7.

Kuhusu uwezekano wa kushindwa kwa idara ya ujasusi ya Israel, Bw. McCaul, mbunge wa Marekani mwenye ushawishi mkubwa, amesema: "Hatujui jinsi tulivyokosa jambo hili, hatujui jinsi gani Israeli ilivyokosea." Maafisa wa utawala wa Biden baada ya mkutano huo "walisita" kuhusisha moja kwa moja Iran katika shambulio la Hamas dhidi ya Israeli, amesema pia.

Hamas, inayotawala tangu mwaka 2007 katika Ukanda wa Gaza na aduimkubwa wa Israel, ilianzisha mashambulizi yake alfajiri siku ya Jumamosi. Kwa jumla, vita hivyo tayari vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,700 kwa pande zote mbili, raia, wanajeshi wa Israel na wapiganaji wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.