Pata taarifa kuu

Israel: 'Serikali ya dharura' yaundwa kwa muda wa vita dhidi ya Hamas

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Benny Gantz, kiongozi wa upinzani, wamefikia makubaliano Jumatano, Oktoba 11, kuunda "serikali ya dharura" kwa muda wote wa vita na Hamas, iliyoanzishwa baada ya mashambulizi ya wpiganaji wa kundi hilo kutoka Palestina mnamo Oktoba 7. Yaïr Lapid hajajumuishwa katika makubaliano haya.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mnamo Septemba 10, 2023 huko Jerusalem.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mnamo Septemba 10, 2023 huko Jerusalem. AP - Ohad Zwigenberg
Matangazo ya kibiashara

 

Mwishoni mwa mkutano kati ya Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, na rais wa Chama cha Umoja wa Kitaifa na Waziri wa zamani wa Ulinzi, Benny Gantz, "watu hao wawili wamekubaliana kuundwa kwa serikali ya dharura na Baraza la kivita," imebainishwa katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari iliyochapishwa alasiri ya Jumatano, Oktoba 11.

Baraza la kivita pia litakuwa chini ya mamlaka ya Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant. Kiongozi mwingine wa upinzani, Yaïr Lapid wa chama cha mrengo wa kati cha Yesh Atid, hakujiunga na taarifa hii kwa vyombo vya habari. Lakini taarifa kwa vyombo vya habari inabainisha kuwa kiti "kitahifadhiwa" kwa ajili yake ndani ya baraza la vita.

"Israel juu ya yote," ameandika Benny Gantz kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) dakika chache baada ya kurasimishwa kwa makubaliano haya kwa serikali ya dharura. Mkuu huyo wa zamani wa jeshi, hasa wakati wa vita vya siku 50 huko Gaza dhidi ya Hamas mnamo mwka 2014, alikuwa Waziri wa Ulinzi kati ya mwaka 2020 na 2022.

Taarifa kwa vyombo vya habari inabainisha kuwa wanachama watano wa chama cha mrengo wa kulia cha Benny Gantz watateuliwa kuwa mawaziri bila mamlaka yoyote. "Hakuna sheria iliyopendekezwa au uamuzi wa serikali usiohusiana na mwenendo wa vita utakaopendekezwa na serikali," taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inabainisha.

Serikali ya sasa ya Benjamin Netanyahu, inayoungwa mkono na wabunge 64 kati ya 120, inaundwa na vyama vya mrengo wa kulia, vya msimamo mkali na vya Orthodox. Kwa kuingia kwa chama cha Benny Gantz, serikali ya dharura itakuwa na uungwaji mkono mpana wa wabunge 76.

Waziri wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben Gvir, ambaye alikuwa amepinga kuundwa kwa serikali hii, alibadilisha upinzani wake na kutangaza kwenye Telegram "kukaribisha umoja", na kuongeza: "Sasa lazima tushinde. "

(pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.