Pata taarifa kuu

Israel kuiangamiza Hamas, nani atasimamia utawala wa ukingo wa Gaza

Israel imejiwekea lengo la kuangamiza vuguvugu la Kiislamu la Hamas lakini mustakabali wa Ukanda wa Gaza unategemea hali ambayo bado haijaeleweka ya Israeli ambayo ina ndoto ya kukata uhusiano wote na eneo la Palestina.

Gaza, eneo dogo la kilomita za mraba 362 lenye wakazi milioni 2.4, tangu wakati huo imekuwa chini ya vizuizi vyaa ardhi, baharini na angani vya Israel na Misri.
Gaza, eneo dogo la kilomita za mraba 362 lenye wakazi milioni 2.4, tangu wakati huo imekuwa chini ya vizuizi vyaa ardhi, baharini na angani vya Israel na Misri. AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

"Jambo moja tu liko wazi, Gaza haitatawaliwa tena na Hamas vita hivi vitakapomalizika," amesema msemaji wa serikali ya Israel Eylon Levy kulingana na shirika la habari la Β AFP, huku jeshi likiharakisha maandalizi yake ya mashambulizi ya ardhini.

Katika hali zote za kuendelea kwa mzozo huo, Israel imetangaza lengo moja tu katika jibu lake kwa mashambulizi ya Oktoba 7 katika ardhi yake yaliyotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina ambalo liliua watu wasiopungua 1,400 kwa mujibu wa mamlaka Israel: "Kuifuta Hamas."

Kundi hili la Palestina lilichukua madaraka huko Gaza mnamo 2007, miaka miwili baada ya Waisraeli kujiondoa katika eneo hili na kufuatia mapambano na Fatah, chama cha rais wa Mamlaka ya Palestina (PA), Mahmoud Abbas.

Eneo hilo dogo la kilomita za mraba 362 lenye wakazi milioni 2.4 tangu wakati huo limekuwa chini ya vizuizi vya ardhini, vya baharini na angani vya Israeli na Misri. Israel, ambayo kwa hakika inadhibiti mipaka ya Gaza, inaonekana na jumuiya ya kimataifa kuwajibika kwa mahitaji ya msingi ya eneo hilo, kama vile chakula.

Chini ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel kwa muda wa wiki tatu ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 4,600, wakazi wa Gaza, karibu 80% yao ambao tayari wana hadhi ya ukimbizi, wanahofia kutoroka eneo hilo mwishoni mwa vita hivi, ikiwezekana kuelekea Misri, na kukumbwa hali mbaya mpya "Nakba" (janga), kama wakati wa Wapalestian walipotoroka Ukanda wa Gaza mnamo mwaka 1948.

Israel haijabainisha nini kitatokea Gaza ikiwa lengo lake la vita litakwa limekamilika. "Tunajadili uwezekano na washirika wetu," amejibu msemaji wa serikali ya Israel kwa shirika la habari la AFP. Katika kipindi cha miaka 16, serikali ya Israel haikuwahi kufikiria kupinduliwa moja kwa moja kwa Hamas, licha ya vita vya hapo awali huko Gaza.

Uhakika pekee ni kwamba Israel haijataja hata mara moja uwezekano wa jeshi jipya na hata kukaliwa kwa kiraia katika eneo hilo. Na hakuna anayeiona Israel yenyewe ikibeba jukumu, mzigo wa kifedha na hatari ya kuwadhibiti moja kwa moja Wapalestina milioni 2.4.

Israel ingependa "kukabidhi funguo" za Ukanda wa Gaza kwa upande wa tatu ambao unaweza kuwa Misri, bila hakikisho lolote kwamba Cairo itakubali hali hii iliyoahirishwa kwa miongo kadhaa, chanzo katika Wizara ya Mambo ya Nje kimeliambia shirika la habari la AFP, ambao inataka kubaki bila kujulikana. Hakuna serikali ya Kiarabu au ya Kiislamu iliyojitokeza katika hatua hii.

Chaguo jingine linaloungwa mkono na kiongozi wa upinzani wa Israel Yair Lapid litakuwa kurejea kwa utawala wa chama cha PA huko Gaza, ambapo Israel inashirikiana chama hicho kusimamia Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. "Lakini kuna matumaini kidogo kwamba chama cha PA, ambacho tayari hakiijapendwa sana, kinaweza kurejea Gaza kufuatia uvamizi wa Israel na kisichukuliwe kama adui," wataalam wa Crisis Group wanasema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.