Pata taarifa kuu

Ukingo wa Magharibi: Emmanuel Macron alaani 'mateso' yanayowakabili wakaazi wa Gaza

Baada ya ziara ya mshikamano nchini Israel ambapo alisisitiza kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas na kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya amani, rais wa Ufaransa amezuru Jumanne hii jioni Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambako amekutana na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Emmanuel Macron ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Magharibi kuzuru makao makuu ya Mamlaka ya Palestina tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7.
Emmanuel Macron ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Magharibi kuzuru makao makuu ya Mamlaka ya Palestina tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7. AP - Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron ndiye kiongozi wa kwanza wa nchi za Magharibi kutembelea makao makuu ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina tangu kuanza kwa vita Oktoba 7 kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina. Kama alivyofanya hapo awali huko Jerusalem, rais wa Ufaransa amesisitiza huko Ramallah juu ya hitaji la "kuanzisha tena mchakato wa kisiasa na Wapalestina", na suluhisho la mataifa hayo mawili. "Hakutakuwa na amani ya kudumu ikiwa hakutakuwa na utambuzi wa haki halali ya watu wa Palestina kwa kuwa na taifa lao huru na serikali. Hakutakuwa na amani ya kudumu ikiwa hakutakuwa na utambuzi wa watu wa Palestina na mamlaka yao ya Taifa la Israeli na umuhimu wa kuwepo kwake na usalama wake, amesisitiza.

"Tunakusihi, rais Macron, kukomesha uchokozi huu," amesema Mahmoud Abbas, akiweka jukumu la mzozo huo kwa Israeli "na nchi zinazoiunga mkono." Bila kutaja Hamas, amelaani mashambulizi ya Israel "ambayo yanaua raia wasio na hatia kwa njia ya kinyama."

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa rambirambi zake kwa "waathiriwa wote wa vurugu zilizosababishwa na shambulio la kigaidi la Hamas".
Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa rambirambi zake kwa "waathiriwa wote wa vurugu zilizosababishwa na shambulio la kigaidi la Hamas". © AFP

Mkuu wa Mamlaka ya Palestina amelaani kwa maneno makali sana mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza "ambayo yanaua raia wasio na hatia kwa njia ya kinyama". Wizara ya Afya ya Hamas inasema watu 5,791 wameuawa tangu Oktoba 7 na kuanza kwa mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Mashambulio haya ya anga ni jibu la shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa lililotekelezwa siku hiyo na Hamas na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1,400, huku watu 200 wakishikiliwa mateka.

Wito wa "ulinzi wa kibinadamu"

"Naona, nasikia mateso ya raia huko Gaza", "hakuna kinachoweza kuwahalalisha", amejibu rais wa Ufaransa. "Maisha ya Wapalestina yana thamani ni sawa maisha ya Wafaransa ambayo yana thamani sawa na maisha ya Waisraeli," ameongeza. Mashambulizi ya Hamas "pia ni janga kwa Wapalestina," Emmanuel Macron amesema. Lakini kama ametoa wito wa "ulinzi wa kibinadamu", hakuenda mbali zaidi na kutaja hadharani "mapatano ya kibinadamu" ambayo yanaweza kufungua njia ya "kusitisha mapigano" siku zijazo, kama ilivyofanya serikali yake siku moja iliyopita.

Emmanuel Macron anatarajia kuenelea na ziara yake hadi Amman ambako, kulingana na ikulu ya Élysée, "pengine" atakutana na Mfalme Abdullah II na "labda viongozi wengine katika ukanda huo" siku ya Jumatano. Ziara ya rais wa Ufaransa inakuja baada ya zile za rais wa Marekani, Joe Biden, au Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak. Alisema katika siku za hivi majuzi kwamba alitaka kwenda Israel wakati ziara yake itakuwa "ya manufaa".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.